May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia afungulia vyombo vya habari

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuvifungulia vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, Ikulu ya Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.

Akigusia sekta ya habari, Rais Samia amesema “wizara ya habari, mnapaswa kusimamia vyombo vya habari, nasikia kuna vyombo vya habari huko mmevifungia, vifungulieni lakini vifuate sheria na kanuni.”

Rais Samia amesema, “tusiwape mdomo mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa habari na nataka kanuni ziwe wazi, ili mtu akifungiwa ajue kosa na adhabu yake. Tusifungie tu kibabe.”

Baadhi ya magazeti yaliyofungiwa ni; MwanaHALISI, Mawio, Tanzania Daima na Mseto.

error: Content is protected !!