Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Chalamila: Samia ameruhusu maandamano Chadema
Habari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Samia ameruhusu maandamano Chadema

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufanya maandamano yao kwa amani bila kuharibu miundombinu ya Jiji hilo kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameruhusu maandamano hayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Chalamila ametoa wito huo leo tarehe 24 Januari 2024, alipowasili maeneo ya Stendi ya Magufuli, Mbezi Mwisho, ambako wafuasi na viongozi wa Chadema wakiongozwa na makamu wao mwenyekiti bara, Tundu Lissu wanatarajia kuandamana kuelekea ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN).

“Mnatakiwa kufikisha ujumbe pale mlipokusudia, serikali tuko na nyie na tunawatakia kila la heri, ninyi na mimi ni wana Dar es Salaam penye mzunguko mkubwa wa pesa, hospitali kubwa na uwekezaji mkubwa, maandamano yetu yanapaswa kulinda uwekezaji wote huo, Rais @samia_suluhu_hassan  na viongozi wote wamesema wacha watu waandamane,” amesema Chalamila.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, alimtaka kiongozi huyo wa Dar es Salaam, kutovuruga maandamano Yao.

Chadema wanatarajia kuanza maandamano Yao katika maeneo mawili, Mbezi Mwisho atakakoongoza Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na Buguruni Sheli atakakoongoza Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Chama hicho kimeitisha maandamano hayo ili kuishinikiza serikali kuiondoa bungeni jijini Dodoma miswada ya marekebisho ya Sheria za uchaguzi, wakidai kuwa ni mibovu.

Pia, wanadai miswada huyo haijabeba mapendekezo yaliyotolewa na wadau kuhusu maboresho ya mifumo ya uchaguzi.

1 Comment

  • Duh! Hongera Mama Dk. Samia Suluhu Hassan. Umeonyesha ukomavu wa kisiasa kutoogopa maandamano kama wakoloni na viongozi waliokutangulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!