Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yampigia ‘saluti’ Prof. Safari
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yampigia ‘saluti’ Prof. Safari

Spread the love

KAULI ya Prof. Abdallah Safari, kwamba Chadema hakiwezi kuingia Ikulu bila kupigania Tume Huru ya Uchaguzi, sasa imevaliwa njuga na chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uongozi mpya wa chama hicho umeeleza, dhamira yake kwanza ya ni Tume Huru ya Uchaguzi, jambo ambalo limekuwa likielezwa na Prof. Safari, alipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema.

Tayari siku tano zimepita baada ya chama hicho kuwa na safu mpya ya uongozi, ambapo Freeman Mbowe, ameendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu akiwa Makamu Mwenyekiti na Mnyika Katibu Mkuu.

Tarehe 22 Desemba 2019, mbele ya wanahabari Mnyika amesema, miongoni mwa vipaumbele vikubwa vya chama hicho ni kupigania Tume Huru, jambo ambali Prof. Safari amekuwa akilihubiri ndani ya chama hicho.

“Ajenda yangu kubwa ilikuwa Tume Huru, Nilimwambia rafiki yangu Lipumba baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995…, nimekuja Chadema sikuona kama kuna msukumo wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

“Kwa hiyo tunataka kwenda Ikulu bila njia ya kwenda Ikulu (Tume Huru), nawaambia kila siku hatuwezi kwenda Ikulu bila Tume Huru…., hata Chadema sijaona nia ya dhati ya kupigania Tume Huru ya Uchaguzi,” alisema Prof. Safari alipofanya mahojiano na Televisheni ya mtandaoni ya MwanaHalisi.

Wiki tatu baada ya kauli ya Prof. Safari, uongozi mpya chini ya Mbowe, Lissu na Mnyika umetangaza kwamba moja ya ajenda kuu kukiwezesha chama hicho kufikia marataijio, ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Mnyika amesema, msukumo wa chama hicho kuanza na Tume Huru ya Uchaguzi, ni kutokana na kuvurugwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba mwaka huu.

“Kutokana na yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kazi ya kwanza na kipaumbele chetu itakuwa ni kudai Tume Huru ya Uchaguzi hadi ipatikane,” amesema Mnyika.

Katibu Mkuu huyo amesema, sasa mkazo wa chama hicho unaelekezwa katika kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kwa maslahi ya umma.

Ajenda zingine zilizotangazwa na uongozi mpya wa Chadema ni pamoja na kuandaa wagombea wa chama hicho kuelekea mwaka 2020, kuandaa ilani ya uchaguzi mkuu ujao, kuendeleza Chadema ni msingi na kuweka utaratibu wa matumizi ya Chadema digitali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!