Thursday , 7 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Ubungo wataabika vitambulisho vya NIDA
Habari Mchanganyiko

Ubungo wataabika vitambulisho vya NIDA

Spread the love

KUKATIKA umeme mara kwa mara, imekuwa changamoto kubwa kwa Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, kupata huduma ya kusajili au kupata namba ya Kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Leo tarehe 23 Desemba 2019 MwanaHALISI ONLINE imefika kwenye kituo cha NIDA kilichopo Kibamba shuhudia baadhi ya wakazi wa manispaa hiyo, wakikwama kupata huduma hizo, kutokana na katizo la umeme.

Baadhi ya wananchi wameilalamikia changamoto hiyo, huku wengine wakilazimika kughairi kuendelea na zoezi hilo, na kuamua kuendelea na shughuli zao.

Anna Emmanuel,  Mkazi Kimara Temboni, amelazimika kuondoka, baada ya huduma hiyo kusitishwa kutokana na katizo la umeme.

“Nilifika asubuhi, nilikuja kufuata namba nimetokea Kata ya Kimara wakaniambia njie huku, nilifuata namba hii mara ya tatu, Waliniambia namba nitatumiwa baada ya mwezi mmoja na nusu, urudi tena au walisema watatuma kwenye simu,” ameeleza Anna na kuongeza;

“Foleni imesimama, wanavyodai hamna umeme, wenyewe wamelala hakuna kinachoendelea mpaka saa hizi . Inabidi niende nikaendelee na shughuli zangu. Sababu hujui unarudi saa ngapi na ikifika saa tisa wanaondoka.”

Asha Juma, Mkazi wa Sinza naye ameamua kusitisha zoezi hilo kwa siku ya leo, na kueleza kwamba atarudi tena kesho tarehe 24 Desemba 2019.

Abdallah Idd Athuman, Mkazi wa Manzese amehoji ofisi ya NIDA kukosa jenereta kwa ajili ya kutatua changamoto ya katatizo la umeme.

“Haiwezekani ofisi kubwa kama hii kukosa jenereta, watu wakae kuanzia asubuhi wanasubiri umeme urudi. Inakuaje ofisi kubwa inakosa jenereta wakati wapiga nakala (Photocopy)  wana jenereta?” Amehoji Athuman.

Athuman ametoa wito kwa mamlaka husika, kutatua changamoto hiyo, ili Wananchi ambao wanafanya kazi za kusafiri nje nchi, waipate huduma hiyo haraka, wakaendelee na majukumu yao.

Nilijiandikisha mwezi wa kumi. Kila tukiuliza kwenye simu wanatupa namba. Wanakuambia ingiza taarifa kwa usahihi. Wanakupa namba ukipiga wanakuambia iko busy. Sasa msaada huo nitaupataje kama ninekosea wangeniambia nimekosea wapi.

“Kazi zetu za magari, dereva huwezi kukaa hapa siku nzima. Huku bosi anakuhitaji, inatakiwa usafiri nje ya nchi, namba hujapata, wanasema laini zitafungwa. Serikali itusaidie,” ameomba Athumani.

MwanaHALISI ONLINE ilitafuta wafanyakazi wa NIDA walioko kituoni hapo, kwa ajili ya ufafanuzi kuhusu suala hilo, lakini walikataa kutoa ushirikiano kwa maelezo kwamba, wao sio wasemaji wa mamlaka hiyo.

Hata hivyo, mmoja wao ambaye hakutaka kutaja jina, alikiri uwepo wa changamoto hiyo. Na kueleza kwamba, Manispaa ya Ubungo inakabiliwa na changamoto ya katizo la umeme, mara kwa mara.

Amesema, leo walianza kutoa huduma ya kutoa namba za NIDA kuanzia saa 1:30 asubuhi, lakini zoezi hilo lilisimama majira ya saa 4:20, umeme ulipokatika.

Mtumishi huyo wa NIDA amesema changamoto hiyo inakwamisha utekelezaji wa majukumu yao, lakini pindi umeme unapokuwepo, hujitahidi kutoa huduma hiyo kwa haraka. Ili kuhudumia wananchi wengi wanaojitokeza.

Wananchi wengi wasiokuwa na namba za NIDA, wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya mamlaka hiyo katika maeneo mbalimbali, ili kupata namba kwa ajili ya kusajili laini zao za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

Msukumo huo umekuja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kuendelea kusisitiza kwamba, itazima mawasiliano ya simu, ambazo laini zake hazijasajiliwa, ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

error: Content is protected !!