Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yawatulia wananchi kuhusu umeme wa REA, vijiji 286 kuwekwa umeme
Habari za Siasa

CCM yawatulia wananchi kuhusu umeme wa REA, vijiji 286 kuwekwa umeme

Katibu CCM Taifa Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wilayani Malinyi
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimesema wakazi wa mijini na vijijini nchini wanapaswa kuwa na subira katika mambo ya maendeleo kwa sababu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu na ipo macho katika kutatua changamoto za wananchi. Anaripoti Christina Haule, Malinyi … (endelea).

Katibu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo aliyasema hayo jana wakati akiwa wilayani Malinyi akiendelea na  ziara yake ya siku tisa mkoani hapa ambapo alisema masuala ya umeme, maji na vingine vipo chini ya Serikali ya CCM ambayo ina nafasi kubwa ya kutatua.

Meneja wa Wakala wa usambazaji nishati ya umeme vijijini (REA) Taifa, Mhandisi Romanus Lwena alisema inatarajia kuweka umeme katika vijiji na vitongoji 286 nchini baada ya kupokea kiasi cha sh Bil 71 kutoka Serikalini ili kusaidia jamii kupiga hatua za maendeleo.

Mhandisi huyo alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka huu ambapo utahusika na kuweka umeme kwenye vituo vya afya 25 vijijini na kwamba kukamilika kwa uwekaji wa huduma hiyo kutatoa fursa kwa wananchi kujitokeza kuomba kupewa huduma.

Meneja REA Taifa Romanus Lwena akijibu mchangamoto za umeme kwa wananchi

Hivyo aliwashauri wananchi kuchangamkia huduma ya umeme inayopelekwa na REA III mzunguko wa pili kwenye makazi yao badala ya kupuuza na kuendelea na maisha yao ya awali huku fedha za Serikali zilizotupwa kwenye mradi huo zikikosa kurejeshwa mapema.

“Tuna mpango wa kuanza kutoa huduma Wilayani, kata, vijiji hadi vitongoji nchini, na hii ni kulingana na uhitaji wa eneo husika, lakini changamoto kubwa ni wanaopewa huduma kuchelewa kuomba kuunganishiwa umeme, nawaomba mjitahidi kuomba huduma hiyo” alisema Mhandisi Lwena.

Aidha Mhandisi Lwena alisema katika kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara baada ya kufungua kituo cha kupooa

Naye Meneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Mhandisi Fadhili Chilombe alisema wameanza utaratibu wa kuweka nguzo za zege ili kupunguza bajeti ya kubadilisha nguo mara kwa mara pale inayotokea changamoto mbalimbali ikiwemo nguzo  kuungua, nguzo kuanguka na mengine.

Alisema tayari nguzo 600 zimeshaanza kuingia ambapo mradi huo utakamilishwa mapema kupitia bajeti ijayo itakapokamilishwa kwa kuwezeshwa na Serikali ya CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!