Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda
Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love

 

MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya mwanamume mmoja kuuawa katika mji mkuu, Kampala kufuatia mzozo wa matokeo ya mechi nchini Uingereza. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mshauri huyo wa vijana alifariki kutokana na majeraha ya kuchomwa kisu baada ya kuingilia kati kuamua zogo la mashabiki baada ya Arsenal kushindwa na Manchester City siku ya Ijumaa.

Allan Kakumba alifariki muda mfupi baada ya kulazwa hospitalini siku iliyofuata, gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Polisi walisema katika taarifa kwamba washukiwa wawili walikuwa kizuizini.

“Tutamfikisha mshukiwa mahakamani hivi karibuni,” Luke Oweyesigire, msemaji wa Polisi wa jiji la Kampala, aliambia BBC.

Bw Oweyesigire alisema Bw Kakumba, 25, aliingilia kati wakati kakake Titus Kyendo, shabiki wa Arsenal, aliponaswa katika vita na wafuasi wa Manchester City.

Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya shabiki wa Arsenal kupigwa hadi kufa huko Adjumani katika wilaya ya West Nile.

Richard Ukuyo alipigwa rungu kisogoni baada ya kumkasirisha mfuasi wa Manchester United aliyeghadhabishwa na ushindi wa Arsenal dhidi yao mwezi uliopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!