Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yaendelea kushusha presha wananchi sakata la bandari
Habari za Siasa

CCM yaendelea kushusha presha wananchi sakata la bandari

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kutumia mikutano ya hadhara kutoa ufafanuzi wa maswali yaliyoibuka kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, juu ya uendeshaji bandari, ili kuondoa utata kwa wananchi juu ya uwekezaji huo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga…(endelea).

Leo Jumatano, tarehe 19 Julai 2023, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Tanga,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewataka wananchi kuiunga mkono Serikali katika mpango wake huo, akisema una lengo la kuongeza mapato.

“Bajeti ya Serikali mwaka huu mfano ni Sh. 44 trilioni, mapato kutoka TRA ambayo ndiyo mkusanyaji wa mapato ni Sh. 26 trilioni , namaanisha kwamba Serikali inabidi itafute trilioni 18 kutoka vyanzo vingine. Kitu gani kitatokea kama tutaruhusu uwekezaji, katika mapato trilioni 26 mapato yatokanayo na bandari ni trilioni 7. Tukifanya uwekezaji yataongezeka kufikia trilioni 26,” amesema Prof. Kitila.

Prof. Kitila amesema wabunge hawakuweka rehani ubunge wao kwa kupitisha azimio la kuridhia mkataba huo,  bali walifanya uamuzi huo baada ya kujiridhisha kwamba uwekezaji ukianza fedha zitapatikana kwa ajili ya kuwapeleka wananchi wao miradi ya maendeleo, hususan afya, elimu, miundombinu ya barabara.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji (PIC), Jerry Silaa amejibu maswali kadhaa kuhusu mkataba huo, ikiwemo linalohoji kama bandari zitauzwa kwa kampuni ya Dubai ya Dubai Port Wolrd, ambapo amejibu akidai mkataba huo hauna lengo la kuuza rasilimali hiyo ya nchi.

Bali Ibara yake ya 2(1), imeweka wazi kwamba una lengo la kuweka msingi wa kisheria wa ushirikiano baina ya Tanzania na Dubai, katika uendeshaji na uendelezaji bandari nchini.

Kuhusu madai ya DP World kuanza kazi katika Bandari ya Dar es Salaam, Silaa amekanusha madai hayo akidai kampuni hiyo haijaanza uwekezaji kwa kuwa Ibara ya 5(2)(3) ya mkataba huo, zinaelekeza miradi kutoanza hadi mikataba ya miradi husika na nchi mwenyeji itakaposainiwa.

Pia, Silaa amesema Ibara ya 1 (a), inatoa ruhusa kwa kampuni ya DP World kwenda bandarini kuangalia mazingira kwa ajili ya kuandaa nyaraka za kuomba mradi.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema Serikali imeamua kutafuta mwekezaji ili kuongeza ufanisi wa shughuli za bandarini kwa ajili ya kupata fedha za kutosha kuhudumia wananchi kupitia miradi ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!