Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG abaini kasoro michezo ya kubahatisha
Habari za Siasa

CAG abaini kasoro michezo ya kubahatisha

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere amebaini ufanisi duni kwenye mchakato wa utoaji leseni kwa waendeshaji wa michezo ya kubahatisha hali inayoweza kuwa hatari kwa wateja wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kichere amebaini hayo kupitia ripoti zake za mwaka 2020/21 alizozifanya akisema, ukaguzi alioufanya kwa mashirika ya udhibiti yenye mamlaka ya kutoa leseni ulibaini mapungufu kadhaa yakiwamo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) kutoa leseni kwa waendeshaji 60 wa michezo hiyo bila ya amana ya kutosha.

Anasema, amana ni kama dhamana ya usalama na ulinzi kwa ajili ya kuwalinda wateja wa michezo hiyo.

Kichere anasema, amana hiyo inaweza kutumika inapotokea waliopewa leseni za uendeshaji wa michezo hiyo wameshindwa kulipa madeni ya wateja wao kama inavyotakiwa na Kifungu cha 18A cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha [kama ilivyorekebishwa mwaka 2019].

“Kwa kutowasilisha dhamana, bodi haiwezi kuwalinda wadau wa michezo ya kubahatisha iwapo waendeshaji wa michezo hiyo wataingia kwenye madeni na wateja wao,” anasema Kichere kwenye ripoti ya Mashirika ya Umma na kuongeza:

“Ninapendekeza Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ihakikishe waendeshaji wa michezo ya kubahatisha wana kiwango cha dhamana cha kutosha ili kulinda wateja iwapo mwenye leseni atashindwa kulipa madeni ya michezo ya kubahatisha.”

Aidha, CAG anasema katika ukaguzi wake “nilibaini Bodi ya Michezo ya Kubahatisha haikufanya ukaguzi kwenye mifumo ya usimamizi wa michezo ya kubahatisha ili kuthibitisha iwapo wenye leseni wanafuata masharti ya michezo hiyo kwa kuangalia masuala kama vile iwapo mifumo imeidhinishwa.

“Mashine za waendeshaji wa michezo ya kubahatisha zimeunganishwa kwenye “seva” na kuangalia iwapo mifumo ilifanyiwa maboresho. Hali hii ni kinyume na Mwongozo wa Ukaguzi wa Bodi wa mwaka 2020 unaotaka kufanyika ukaguzi katika eneo la shughuli za michezo ya kubahatisha nchini.”

Anasema ni muhimu kwa bodi kufanya ukaguzi ili kutathmini uzingatiaji wa sheria za michezo ya kubahatisha na mahitaji mengine ya udhibiti ili kuhakikisha kuna usimamizi unaofaa wa tasnia ya michezo ya kubahatisha.

“Kukosekana kwa ukaguzi wa mifumo inayotumika kwenye michezo ya kubahatisha kunaondoa uhakika wa mifumo hiyo, hivyo kunaweza kusababisha upotevu wa mapato yanayotarajiwa kutokana na shughuli za michezo ya kubahatisha,” anasema na kuongeza:

“Ninapendekeza Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) ifanye mapitio ya rasilimali za kitengo chake cha ukaguzi wa michezo ya kubahatisha ikiwa pamoja na kuwa na wakaguzi wa mifumo ili kiweze kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mifumo ya michezo ya kubahatisha.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!