Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara Benki ya NBC yazindua kampeni kuhamasisha kilimo cha ufuta Lindi
Biashara

Benki ya NBC yazindua kampeni kuhamasisha kilimo cha ufuta Lindi

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la Ufuta mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Jaza Kibubu Uvune’ inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la ufuta katika mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Lindi jana. Waliopo meza kuu ni pamoja na Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC, Alelio Lowassa (Katikati)
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni maalum kwa wakulima wa zao la Ufuta katika mkoa wa Lindi inayofahamika kama ‘Jaza Kibubu Uvune’ inayolenga kuhamasisha wakulima hao kujiwekea akiba kupitia benki hiyo huku wakipata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli na pikipiki. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Hatua ya benki hiyo imeungwa mkono na serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ambaye amebainisha kuwa kupitia kampeni hiyo wakulima wa zao la ufuta mkoani Lindi watahamasika zaidi kuwekeza juhudi zao kwenye kilimo cha zao hilo la kimkakati huku pia wakiendelea kujijengea utamaduni wa kutunza akiba.

Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC, Alelio Lowassa akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la Ufuta mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Jaza Kibubu Uvune’ inayoendeshwa na benki hiyo mahususi kwa wakulima wa zao la ufuta katika mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Lindi jana.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jana tarehe 14 Aprili, 2022 mkoani Lindi na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika pamoja na wakulima, Ndemanga alisema hatua ya benki hiyo inakwenda sambamba na mkakati wa mkoa huo katika kuhamasisha kilimo cha mazao ya kimkakati ikiweko ufuta na korosho.

“Kwa hapa Lindi, zao la ufuta ni zao la pili kibiashara baada ya korosho na sisi ndio wazalishaji wakubwa wa ufuta hapa nchini. Ujio wa kampeni hii utatusaidia sana kutuwezesha tuendelee kuwa vinara zaidi kwa kuwa sasa wakulima watahamasika zaidi na pia itavutia hata wale ambao sio wakulima wa zao hili nao pia waingie rasmi kwenye kilimo hiki…tunawashukuru sana NBC,’’ alisema.

Aidha, Ndemanga alitoa wito kwa wakulima hao kuweka akiba zao kupitia benki hiyo ili wanufaike zaidi.
Awali akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC, Alelio Lowassa alisema inalenga kuunga mkono maelekezo ya Serikali yanayozitaka taasisi za fedha nchini kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwa kubuni huduma zinazolenga kumsaidia zaidi mkulima.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la Ufuta mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Jaza Kibubu Uvune’ inayoendeshwa na benki hiyo mahususi kwa wakulima wa zao la ufuta katika mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Lindi jana.

“Kupitia kampeni hii wakulima watakaojiwekea akiba kuanzia kiasi cha sh 500,000 kwenye ya akaunti zao za NBC Shambani watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia baiskeli na pikipiki kupitia droo zitakazofanyika kila baada ya wiki mbili ndani ya miezi mitatu ya kampeni hii.’’ alibainisha.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao Mwenyekiti wa AMCOS ya Tulinde ya Wilayani Tandahimba Bw Mustapha Rashid Salehe alisema pamoja na kuwahamasisha wakulima wa zao la ufuta kujiwekea akiba kupitia benki hiyo, kupitia kampeni hiyo wakulima hao watahamasika zaidi kuongeza juhudi katika uzalishaji wa zao hilo la ufuta kupitia zawadi mbalimbali zitakazotolewa ikiwemo baiskeli na pikipiki.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (wanne kulia – mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa zao la Ufuta mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Jaza Kibubu Uvune’ inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa zao la ufuta katika mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Lindi jana.

“Naamini kampeni hii itatuongezea sana ari ya kuendelea kulima zao la ufuta kwasababu tunaamini nyuma yetu tunaungwa mkono na taasisi kubwa za kifedha kama NBC ambayo kupitia kampeni hii itatuwezesha kutunza fedha zetu bila makato yoyote huku pia tukiwa kwenye nafasi ya kujishindia baiskeli na pikipiki. Binafsi sina mashaka na kampeni hizi za NBC kwa kuwa tayari nilikwisha nufaika na kampeni yao iliyokwisha ya Vuna Zaidi na NBC Shambani ambapo nilijishindia pampu ya kupulizia dawa mikorosho yangu,’’ alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!