Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Bunge Poland lapewa ”meno” kufukuza majaji
Kimataifa

Bunge Poland lapewa ”meno” kufukuza majaji

Bunge la Poland
Spread the love

BUNGE la taifa nchini Poland limepitisha muswaada unaolipa nguvu ya kuteua au kutengua viongozi wa mahakama kuu wakiwemo majaji wa juu, anaandika  Catherine Kayombo.

Muswaada huo uliopitishwa na wabunge kutoka chama tawala cha PIS na washirika  wao kwenye serikali ya mseto umesomwa kwa mara ya kwanza jana, Julai 19 na sasa kamati ya bunge inatazamiwa kuujadili kwa haraka.

Hatua hiyo imepata upinzani mkali kutoka kwa wananchi na wabunge wa upinzani na wamekosoa bunge kwa kudai linaingilia uhuru wa mahakama katika kusimamia haki za binadamu.

Usiku wa kuamkia leo, maelfu ya waandamanaji wa upinzani walikusanyika nje ya viwanja vya bunge wakipinga kupitishwa kwa sheria hiyo, hali iliyopelekea jingo la bug e kulindwa kwa vizuizi na walinzi wa serikali.

Kiongozi wa maandamano hayo, Pawel Kasprzak, amesema muswaada huo unamaanisha kwamba kanuni ya utenganishaji wa madaraka kwenye demokrasia ya Poland kwani hatua hii ni nia ya bunge kuweka udhibiti wake dhidi ya mahakama.

Kupitishwa kwa muswaada huo, kamisheni ya umoja wa Ulaya imetiwa wasiwasi na hatua ya serikali ya Poland kutaka kudhibiti mahakama kupitia bunge hivyo, imeitisha mkutano na kiongozi wa Poland rais Andrzej Duda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!