August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar yanasa 44 wizi wa magari

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya (wakwanza) na kulia ni muonekano wa gari lililong'olewa baadhi ya vifaa

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limewakamata watuhumiwa 44 wa wizi wa vifaa vya magari pamoja na vifaa hivyo vya magari,  katika oparesheni maalum inayoendelea, anaandika Irene David.

Lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha wezi hao pamoja na wanunuzi wa vifaa hivyo sehemu mbalimbali jijini hapa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam, Lucas Mkondya, ameyasema hayo leo hii wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo makao makaoni hapa.

Watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kupekuliwa katika maduka yao na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari vikiwemo, ‘Side Mirrors’ 105, Vitasa vya Magari 136, ‘Wiper Switch’ saba, Bampa nne,’Left Pump’ moja, ‘Air Cleaner’ moja,’Booster’ tatu, ‘Show Grill’ sita, Mashine ya kupandishia vioo moja na ‘Tyre Used’.

Mkondya amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya ‘Browing’ patent ikiwa na risasi tisa baada ya majibizano ya risasi kati ya askari polisi na jambazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Adam ambaye alifariki dunia katika majibizano hayo.

Wakati huo huo, Mkondya amesema kuanzia tarehe 17.07.2017 hadi 19.07.2017 kikosi cha usalama barabarani kimefanikiwa kukamata magari 5,592, Pikipiki 342, Daladala 2,049, Malori 3,543, Bodaboda 22 kwa kosa la kupandisha mishikaki.

Mkondya amewashukuru wananchi kwa kutoa taarifa ya wahalifu na linawaomba wananchi waendelee kutoa taarifa ili jiji liendelee kuwa salama.

error: Content is protected !!