Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Bosi NMB arejea shule aliyosoma, awafunda wanafunzi
Habari

Bosi NMB arejea shule aliyosoma, awafunda wanafunzi

Spread the love

 

BAADA ya kuondoka shule ya sekondari ya wasichana wenye vipaji ya Kilakala, mkoani Morogoro miaka 30 iliyopita akiwa mhitimu wa kidato cha nne, Ruth Zaipuna amerejea shuleni hapo akiwa ni afisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB na kuwapa siri ya kufikia mafanikio. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Ruth alihitimu kidato cha nne shuleni hapo, amewamegea mambo manne makubwa wanafunzi hao yaliyomfanya kufikia nafasi anayohudumu sasa kwenye benki hiyo inayoongoza nchini na kuwataka nao kuyatumia ipasavyo.

Bosi huyu wa NMB alibainisha hayo mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 59 ya kidato cha nne shuleni hapo. Jumla ya wanafunzi 88 wanatarajiwa kufanya mtihani wa taifa itakayoanza tarehe 15 Novemba hadi 2 Desemba 2021.

Alisema, ili kufikia mafanikio yanahitaji kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na kufanya kazi kwa bidii.

Pia, kuwa mwaminifu na mwadilifu ndio moja ya nguzo katika jambo lolote alifanyalo mwanadamu iwe katika elimu, kazi majumbani au kuajiriwa, kujiajiri huku akiitaka jamii kufanya yote kwa bidii, uadilifu na uadilifu kwani hiyo ni njia ya mafanikio.

“Nidhamu ni jambo la msingi na muhimu mno hivyo ni nidhamu pekee itayokuwezesha kutawala maisha yako na kuwa na mahusiano bora na wengine lakini kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu ni silaha nyingine,” alisema Ruth

Ruth alisema yeye ambaye ni mwanafunzi aliyesoma shuleni hapo miaka 30 iliyopita na wao kama benki ya NMB wataendelea kutilia mkazo jukumu lao la uwajibikaji katika jamii kwa nyanja mbalimbali ikiwemo eneo ya elimu, afya, majanga yanayoikumba nchi kama mafuriko na vimbunga vinavyoathiri wananchi.

“Sambamba na sera yetu ya uwajibikaji kwa jamii, benki yenu ya NMB inatoa meza 50, viti 50 vyenye thamani ya Sh.5 milioni pamoja na kompyuta 10 aambazo tuna uhakika zitakuwa chachu ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na ufundishaji shule hapa,” alisema Ruth

Alitumia fursa hiyo, kuwasihi wanafunzi kuhakikisha wanaweka mkazo kwenye masomo yao na wanaokwenda kufanya mitihani kujiandaa vyema “kwa kumtanguliza Mungu mbele” ili wafanye vyema na kufaulu.

Ruth amewataka wanafunzi kuwa na malengo ya kipi wanataka kukifanya baada ya kuhitimu masomo yao na kujiepusha na mambo ambayo hayana tija kwao kwa sasa.

Kwa upande wake, Doreen Patrick, akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake, alibainisha changamoto kadhaa zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na upungufu wa viti na meza vya kusomea.

Pia, kuna upungufu wa viti na meza vya bwaloni huku uchakavu wa ukumbi wa Nyerere Hall, uhalibifu wa milango ya madarasa na mabweni na kukosekana nishati mbadala pindi umeme unapikatika.

Awali, Mkuu wa Shule ya Wasichana Kilakala, Mildreda Selula alisema, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 657 huku wanafunzi wanaohitimu wakiwa 88.

Mildreda alisema shule hiyo ina michepuo ya sayansi, biashara na sanaa kwa kidato cha kwanza hadi nne na kidato cha tano na sita kukiwa na tahasusi tatu za sayansi ambazo ni PCM, PCB, CNG pamoja na tahasusi moja ya sanaa ambayo ni HGL.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

ElimuHabari

Shule ya Hazina yaanza kutoa elimu bure

Spread the loveKATIKA jitihada za kuunga mkono serikali ya awamu ya sita...

AfrikaHabari

Majenerali 35 kustaafu kutoka jeshi la Uganda

Spread the loveTAKRIBANI majenerali 35 wanatarajia kustaafu kutoka jeshi la Uganda (UPDF)...

error: Content is protected !!