Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara BetPawa, Polisi waungana kutoa mafunzo  ya usalama barabarani kwa bodaboda
BiasharaHabari Mchanganyiko

BetPawa, Polisi waungana kutoa mafunzo  ya usalama barabarani kwa bodaboda

Spread the love

ZAIDI ya waendesha bodaboda 250 mkoani Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya usalama barabarani yalioandaliwa na kutolewa na Kampuni ya BetPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kitengo cha usalama barabarani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Meneja Masoko wa  kampuni ya BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu (kushoto) pamoja na SP Deus Sokoni, Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, wakimkabidhi cheti cha ushiriki Boniface Matale mmoja kati ya madereva boda boda 250 aliyeshiriki katika mafunzo ya usalama barabarani kwa mkoa wa Dar es Salaam. Anayeshudia kushoto ni Koplo Rashid Msuya kutoka dawati la elimu jeshi la Polisi

Mafunzo hayo yanayojulikana kama ‘betPawa na  elimu ya Usalama Barabarani’ yanalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupiga vita ajali za barabarani zinazoweza kuepukika na ambazo husababisha majeraha na vifo haswa kwa waendesha bodaboda ambao wamekuwa ni moja kati ya kundi linaloathirika sana.

Akizungunza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja masoko wa betPawa Tanzania Borah Ndanyungu alisema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa bodaboda ni kundi ambalo limekuwa likichangia sana katika ajali za barabarani huku akitaja  uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali hizo.

Sajenti Asha Abdul kutoka makao makuu ya Polisi akizungumza wakati wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa boda boda 250 wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

“Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 16,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani huku ajali za bodaboda zikichukua nafasi kubwa. Kutokana na ukweli huu, tumeona kuna haja ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kundi hili ambalo limekuwa ni muhanga wa ajali za barabarani,” alisema.

 Mwakilishi wa waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam Boniface Mtale alisema ajali za bodaboda zimekuwa zikiongezeka kwa kasi na kufafanua kuwa uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarani zimekuwa ndiyo chanzo kikuu cha ajali hizo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya kubashiri michezo ya BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani kwa bodada 250 wa mkoa wa Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na BetPawa kwa kushirikiana na Polisi, kitengo cha usalama barabarani na yamefanyika mwishoni mwa wiki.


“Uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarabi bado ni changamoto kubwa kwa madereva wengi wa bodaboda. Tunawashukuru sana BetPawa  kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutambua tatizo hili na kuamua kutupatia elimu hii muhimu sana kwetu,” alisema

 Kwa upande wake SP Deus Sokoni ambaye ni Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, aliipongeza kampuni ya kubashiri michezo ya BetPawa kwa kudhamini mafunzo hayo muhimu

 “Sisi sote kwa pamoja ikiwa ni Pamoja na jeshi la Polisi, madereva, jamii nzima na wadau wote tuna wajibu wa kufanya barabara zetu ziwe salama. Ninayofuraha kuona BetPawa wamekuwa mstari wa mbele na kuamua kufadhili mafunzo haya ambayo yatasaidia sana kundi hili la bodaboda.,

 Aliongeza, ajali za barabarani zinsababisha hasara kubwa kwa taifa,  familia na jamii kwa ujumla. Hasara hizi ni Pamoja na kupoteza wapendwa wetu ambao wengine tunawategemea, ulemavu wa kudumu pamoja na gharama kubwa za matibabu kwa wahanga wa ajli. Kwa Pamoja tukiungana tunaweza kupunguza sana kama siyo kumaliza kabisa tatizo hili,”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!