Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo yaanika mapendekezo mkataba DP World
Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika mapendekezo mkataba DP World

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetoa mapendekezo namna ya kuboresha mkataba wa ushirkiano wa kiserikali (IGA), kati ya Serikali ya Tanzania na Imarati ya Dubai, kuhusu uwekezaji bandarini, ili kuondoa utata uliobuka miongoni mwa wananchi juu ya maslahi itakayopata Tanzania kupitia uwekezaji huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mapendekezo hayo yamewasilishwa leo tarehe 4 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam na viongozi waandamizi wa chama hicho, akiwemo Makamu Mwenyekiti Bara, Dorothy Semu na Katibu Mkuu, Ado Shaibu, baada ya kamati yake maalum iliyounda kufanyia kazi masuala yaliyoibuliwa na jamii juu ya mkataba huo, kumaliza kazi yake.

Wakitoa mapendekezo hayo, viongozi hao wameitaka Serikali iwasilishe taarifa ya marekebisho ya makubaliano hayo kwa Serikali ya Dubai, ili yafanyike kabla ya kusaini kwa mkataba wa nchi mwenyeji kati ya Tanzania na DP World.

Wakichambua dosari za mkataba huo, viongozi hao wamedai kamati ilibaini maeneo kadhaa yenye kasoro, ikiwemo  ibara ya kwanza ya IGA inayotoa nafasi kwa kampuni ya Dubai Port World (DP World), kuanzisha kampuni moja au zaidi, kwa ajili ya utekelezaji miradi nchini.

Wanadai ibara hiyo haitoi fursa ya ushiriki katika uwekezaji huo kwa wananchi au kampuni za ndani, kwa kuwa hailazimishi kampuni zitakazoanzishwa ziwe na sehemu ya umiliki wa watanzania ama kupitia kampuni ya umma au binafsi.

Kufuatia dosari hiyo, wamesema ACT-Wazalendo kimependekeza iundwe kampuni maalum ya umma itakayoingia ubia na DPW kuendesha shughuli zote za miradi katika ushirikiano huo.

“Ubia unaopendekezwa uwe ni wa Kampuni maalumu ya Umma kumiliki mpaka 50% ya hisa zote za Kampuni ya Ubia.”

Pia, chama hicho kimedai uchunguzi wake umebaini dosari katika makubaliano ya kampuni hiyo kufanya shughuli za awali kabla ya miradi husika na kushauri “kuhusu shughuli za mwanzo za mradi kuwe na mkataba maalum na Mamlaka za Ndani utakaongoza shughuli hizo,”

“Pia kuwezesha DPW kupata taarifa za kiutafiti wa kimazingira kwa upande mmoja na pia kuwezesha Serikali kujua na kuthibitisha gharama na upeo wa shughuli hizo ili kuepuka sitofahamu ya upeo wa kazi za awali na gharama zake.”

Katika hatua nyingine, chama hicho kimeitaka Serikali iweke wazi mchakato uliotumika kuipata kampuni ya DP World, ili wananchi wafahamu na kujiridhisha kuwa utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

Ibara ya 4 (2) ya mkataba huo, imedaiwa kuwa na dosari kwa maelezo kwamba inaipoka nchi uhuru wa kuamua, kwa kuwa inaielekeza nchi kuipa taarifa Imarati ya Dubai kuhusu fursa yoyote inayohusiana na bandari.

Hivyo chama hicho kimeshauri “Ibara hii ifutwe na DPW ipewe haki ya kushiriki kwenye zabuni iwapo kutakuwa na miradi mingine ambayo Serikali itaamua kuanzisha ili washindane na wawekezaji wengine na Tanzania ichague Mwekezaji atakayewashinda wengine kwa vigezo vitakavyowekwa.”

Katika hatua nyingine, ACT-Wazalendo kimeshauri DP World isipewe zabuni za kuendesha shughuli za bandari katika gati zilizokuwa chini ya Kampuni ya TICTS na gati mpya zitakazojengwa, bali zitafutwe kampuni nyingine zifanye uwekezaji huo kwa lengo la kuweka ushindani wa waendeshaji.

Wakati huo huo, ACT-Wazalendo imependekeza ibara ya 5 (1) ya mkataba huo ifutwe, kwa kuwa inaipa haki ya kipekee DP World katika kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi yote, kitendo kinachodaiwa kuibana Serikali ya Tanzania kuwa na wajibu wa kutofanya ushirikiano na mashirika mengine juu ya suala hilo.

Kasoro nyingine iliyotajwa na ACT-Wazalendo katika mkataba huo, ni kutotaja muda wa ukomo ambapo ibara yake ya 23 (1), inaeleza ukomo wa makubalianmo hayo utatokea pale ambapo shughuli za miradi zitafika mwisho

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!