Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 18 wahitimu mafunzo ya ukurugenzi
Habari Mchanganyiko

18 wahitimu mafunzo ya ukurugenzi

Spread the love

WASHIRIKI 18 wa mafunzo ya nafasi ya ukurugenzi, mkuu, wamehitimu Program ya Mpango wa Uandaaji Wakurugenzi Watendaji (CAP), awamu ya tatu inayoratibiwa na Jukwaa la Wakurugenzi Wakuu (CEOrt). Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti CEOrt, David Tarimo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya tatu ya wahitimu hao ambapo aliweka bayana kuwa asilimia 60 ni wanaume na 40 wanawake.

Mwenyekiti wa Program ya CAP Brenda Msangi akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Derm Constructions, Ridhiwan Mringo

Tarimo alisema CEOrt ilianzisha mafunzo hayo ambayo yanashirikisha washiriki kutoka sekta ya umma na binafsi yamekuwa na mafanikio kwa kuweza kujenga uwezo wa washiriki kupanda cheo baada ya kupata mafunzo hayo.

Alisema katika mafunzo haya ya 2023 kati ya washiriki 18, watano wanatoka sekta ya umma, jambo ambalo linawapa nguvu ya kuendeleza program hiyo.

“CEOrt imekuwa ikiandaa wakurugenzi wakuu wajao tangu mwaka 2019 ambapo mwaka huu ni awamu ya tatu na washiriki 18 wameshiriki na kuhitimu, hivyo tumekutana hapa kuwapongeza, ili waende kutumikia taifa,” alisema.

Tarimo alisema CAP ilizaliwa kutokana na uhitaji wa wakurugenzi wakuu ambao ulikuwepo, hivyo wakalazimika kukuza vipaji vya ndani kuingia katika nafasi za uongozi wa juu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya CEOrt na Mwenyekiti wa Program wa CAP, Brenda Msangi alisema program hiyo inalenga wakurugenzi na maofisa waandamizi ambao wanaripoti kwa wakurugenzi wakuu, hivyo wanapata maandalizi ya kuwa wakurugenzi wakuu.

Mwenyekiti huyo alisema katika kutambua pengo lililopo katika uongozi na haja ya uwekezaji zaidi katika mtaji wa binadamu wa Tanzania, CEOrt ilishirikiana na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Strathmore (SBS) kuzindua mpango maalum wa uongozi huu mwaka 2019.

Alisema wahitimu hao wanafanya program za jamii ambazo zinaweza kusimama zenyewe na kujiendesha, hali ambayo inatoa picha sahihi pale wakipata nafasi ya ukurugenzi hawatatetereka.

Msangi alisema mafunzo hayo ya kuandaa wakurugenzi yalianza na washiriki 16 mwaka 2019, sita 2021na 18 2023 na inayokuja hadi sasa washiriki waliomba ni 20.

“Tangu program hii ianze mwaka 2019 hadi sasa wapo washiriki wa mafunzo nane wamefanikiwa kupata nafasi ya kuwa wakurugenzi wakuu na matokeo yake yanaonekana mazuri ndani ya nchi na Afrika kwa ujumla,” alisema.

Msangi amewataja wanufaika ambao kwa sasa wanaongoza taasisi ni Anael Samuel, Mkurugenzi Mtendaji wa Songas, Julius Ruwaichi, Mkurugenzi Mtendaji wa Access Bank, Unguu Sulay, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Alimiya Osman Munge, Mkurugenzi Mtendaji wa Faru Graphite Corporation Ltd na Resham Vassa, Mkurugenzi Mtendaji wa Reni International

Wengine ni Shreekesh Karia, Mkurugenzi Mtendaji wa DHL East Africa, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, na Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Tanzania aliyeteuliwa hivi karibuni, Manzi Rwegasira

Mwenyekiti huyo alisema dhamira yao ni kuwezesha watu wote wenye sifa za kuwa wakurugenzi wanapata nafasi ya kusoma CAP ili waweze kuwa viongozi sahihi.

“Lengo kuu la mpango wa CAP linabaki kuwa: kutambua na kuwavuta wakurugenzi wakongwe wenye njia ya kazi kuelekea nafasi za mkurugenzi mtendaji, hivyo kuunda mkondo wa viongozi wanaoaminika na wenye mtazamo wa mbele nchini Tanzania,” alisema.

Alisema tangu kuanzishwa CAP Serikali ya Tanzania, imekuwa ikitoa ushirikiano, huku ikisisitiza dhamira ya ushirikiano katika kuendeleza kizazi kipya cha viongozi wenye uwezo na mtazamo wa mbunifu kwa ustawi wa taifa.

Alisema kuwekwa kwa uongozi wa Tanzania wenye uwezo katika sekta muhimu kama mafuta na gesi, benki, na utengenezaji imechangia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha maendeleo ya uchumi wa ushindani na wa viwanda.

“CAP imefanikiwa kuongeza ushiriki wa wanawake kwa asilimia 100 katika mpango huo. Kama sehemu ya moduli, miradi ya athari ya kijamii inaleta ubunifu na imepelekea uzinduzi na utambulisho wa suluhisho endelevu maarifu yanayojibu changamoto muhimu za kijamii na kiuchumi,” alisema.

Alisema CEOrt inashukuru Kamati ya Utekelezaji wa CAP na wadhamini wa mpango wakiwemo A&K Tanzania Limited, Vodacom Tanzania, Sportspesa Tanzania Ltd, Oryx Gas, Kampuni ya Sigara ya Tanzania na Benki ya NBC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!