Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki Ya NBC Yafungua Milango Zaidi Kwa Wafanyabiashara Wa Tanzania Na Afrika Kusini
Habari Mchanganyiko

Benki Ya NBC Yafungua Milango Zaidi Kwa Wafanyabiashara Wa Tanzania Na Afrika Kusini

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu utayari wake katika kufanikisha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Afrika kusini kupitia huduma zake hususani kwa katika uwekezaji wa biashara na kilimo.

Msimamo huo wa benki hiyo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini, Manish Thakrar (katikati) akizungumza na wajumbe wa jukwaa hilo wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

 Sabi alisema kwa muda mrefu sasa benki hiyo imekuwa mdau mkubwa wa wafanyabiashara kati ya Afrika Kusini na Tanzania ambapo kupitia mkutano huo aliweza kuelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara hao ikiwemo huduma za huduma za mikopo ya biashara na kilimo.

“Jukumu letu kama benki kubwa hapa nchini ni kuhakikisha tunatoa masuluhisho ya kibiashara kwa wafanyabiashara wetu ili waweze kufanya shughuli zao kiushindani ndani na  nje ya nchi. Tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwao ikiwemo mikopo ya aina mbalimbali ikiweo ya biashara na kilimo, bima kupitia benki sambmba na kuhusumia mnyororo wote wa biashara ikiwemo kuhifadhi fedha, kutuma na kupokea fedha kutoka ndani nan je ya nchini,’’ alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini, Manish Thakrar wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini,  Bw.  Manish Thakrar alisema umuhimu wa benki ya NBC na taasisi nyingine za kifedha ni mkubwa hususani katika kipindi hiki ambacho kuna ongezeko kubwa la biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini.

“Tunawashukuru sana NBC tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kwasasa tunawahitaji zaidi. Changamoto ya COVID 19 pamoja na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine imeongeza sana mahitaji ya bidhaa hususani za vyakula nchini Afrika Kusini hivyo kwetu hiyo inaweza kuwa fursa kubwa ikiwa tutachangamkia. Hata hivyo habari njema ni kuwa benki ya NBC imeonyesha kutoa kipaumbele pia kwenye mikopo ya kilimo hilo litatusaidia sana kwa kuwa bidhaa za vyakula zinahitajika zaidi huko Afrika Kusini,’’ alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!