Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bendera za CUF zachomwa moto
Habari za Siasa

Bendera za CUF zachomwa moto

Spread the love

CHAMA Cha Wananchi (CUF) chini ya mwenyekiti wake Prof. Ibrahim Lipumba kimeanza kupita kwenye wakati mgumu baada ya Maalim Seif Shariff Hamada, aliyekuwa katibu wake kuhamia ACT-Wazalendo leo tarehe 18 Machi 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ni kutokana na baadhi ya wanachama wa CUF waliokuwa wanamuunga mkono Maalim Seif kuanza kuchoma moto bendera za chama hicho.

Tukio hilo limetokea leokatika ofisi za CUF Wilaya ya Tanga Mjini, ikiwa ni muda mfupi baada ya Maalim Seif kutangaza kwamba yeye na wafuasi wake wanahamia ACT-Wazalendo.  

Taarifa zalizothibitishwa na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma CUF, Mbarara Maharagande, zinaeleza kuwa, baadhi ya wafuasi wa chama hicho katika mikoa ya Unguja na Pemba wameshusha bendera za chama hicho na kupandisha bendera za ACT-Wazalendo.

Maalim Seif alitangaza kuhamia ACT-Wazalendo yeye pamoja na wafuasi wake baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa uamuzi wa kesi Na. 23/2016 iliyokuwa inapinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia maamuzi ya ndani ya CUF, pale alipotangaza kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama, inaeleza kuwa msajili alikuwa na mamlaka ya kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF licha ya kujiuzulu wadhifa huo.

Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesema kambi yake ilifanya kazi kubwa kukitetea chama hicho, lakini haikuwa kazi ya lelemama kufanikisha hilo jambo.

“Nimalizie kwa kuwaambia Watanzania kuwa mapambano ya kujenga demokrasia na kusimamisha utawala wa haki unaoheshimu utawala wa sheria si kazi ya lelemama. Tumefanya kazi kubwa mpaka hapa tulipofikia. Ni jukumu letu na wajibu wetu sasa kuikamilisha kazi hiy,” amesema Maalim Seif.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni, kambi ya Prof. Lipumba ilifanya mkutano wake mkuu wa saba jijini Dar es Salaam, ambapo wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa lilimteua Halifa Suleiman Halifa kushika wadhifa wa Maalim Seif.

Mgogoro wa kiuongozi ndani ya CUF umefikia tamati kufuatia hatua ya Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo, baada ya kufukuta kwa miaka minne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!