Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Koffi Olomide akumbwa na jinai ya ubakaji
Michezo

Koffi Olomide akumbwa na jinai ya ubakaji

Spread the love

NYOTA wa muziki wa Rhumba nchini Kongo, Antonie Agbepa Mumba maarufu kwa jina la Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini katika Mahakama ya Nanterre nchini Ufaransa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mnenguaji wake wakati akiwa na umri wa miaka 15. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hukumu hiyo iliyotolewa jana tarehe 18 Machi 2019 na Mahakama ya Nanterre ambapo pia ilimtaka Olomide (62) kulipa faini yenye kiwango sawa na gharama za kuwasaidia wanawake watatu wengine walioingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.

Pia, ilimtaka kumlipa mnenguaji huyo Euro 5,000 kama fidia ya madhara aliyomsababishia alipomfanyia ukatili huo.

Mnamo mwaka 2012 Olomide alifunguliwa mashtaka ya ubakaji na wanenguaje wake wanne, wakimtuhumu mbele ya mahakama kwamba aliwanyanyasa kingono katika nyakati tofauti mwaka 2002 na mwaka 2006 nchini Kongo na Ufaransa.

Katika malalamiko yao, wanenguaji hao waliiambia mahakama hiyo kuwa Olomide aliwazuia kwa lazima nyumbani kwake iliyoko nje ya mji wa Paris nchini Ufaransa,  na kwamba walifanikiwa kutoroka licha ya kwamba walishindwa kurudi Kongo kutokana na kuogopa kutafutwa na kulipizwa kisasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!