Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto atinga ofisi za CUF, ajifungia na Maalim Seif
Habari za Siasa

Zitto atinga ofisi za CUF, ajifungia na Maalim Seif

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 18 Machi 2019 amefika katika Ofisi ya Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) Magomeni jijini Dar es Salaam kuzungumza na Maalim Seif Shariff Hamad. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo alifika ofisini hapo muda mfupi baada ya Maalim Seif, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF kutangaza kujiunga na ACT-Wazalendo.

Kufika kwa Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini kulipokewa kwa shangwe na baadhia ya viongozi waliokuwa wa CUF na wanaomuunga mkono Maalim Seif.

“ACT-Wazalendoooo, ACT-Wazalendoo” ndio maneno yaliyokuwa yakitamkwa na viongozi hao wakati wakimpokea Zitto ambaye baada ya kufika, alipelekwa moja kwa moja chumba alichokuwemo Maalim Seif.

Humo ndani Zitto na Maalim Seif walitete kwa dakika kadhaa na kisha Zitto kutoka na kupanda gari lake kisha kutokomea. Haijaelezwa Zitto na Maalim Seif walizungumza nini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!