Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani
Habari za Siasa

Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani

Sharifa Suleiman, Makamu wa Bawacha-Zanzibar
Spread the love

 

BARAZA la Wanawake wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Bawacha), nchini Tanzania, limesitisha kongamano la ‘Siku ya Wanawake Duniani’ kitaifa, lililopangwa kufanyika mkoani Iringa, 8 Machi 2021. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Sababu zilizosababisha kuahirishwa kwa kongamano hilo, ni kuzuia maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Uamuzi wa kuahirisha, ulifikiwa jana Jumatatu tarehe 1 Machi 2021, katika kikao cha kamati ya utendaji ya Bawacha, iliyokutana kwa njia ya mtandao.

“…imefikia uamuzi huo, ikiwa ni jitihada mojawapo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 (matatizo kwenye mfumo wa hewa wa binadamu), yanayosababisha vifo kwa wapendwa wetu,” amesema Sharifa Suleiman, makamu wa Bawacha-Zanzibar, kupitia taarifa yake kwa umma

Amesema, zaidi ya wanawake 3,000, kutoka mikoa mbalimbali nchini, walikuwa wamethibitisha kushiriki hivyo, itakuwa vigumu kuepuka msongamano, kutokana na tukio lenyewe.

Sharifa amesema, hali itakaporuhusu mkusanyiko mkubwa kama huo, Bawacha itatangaza mahali na tarehe rasmi ya kungamano jingine maalum ambalo, litakutanisha wanawake wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!