September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bavicha na UV-CCM, ni pipa na mfuniko

John Pambalu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha)

Spread the love

BARAZA la taifa la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo ((BAVICHA), jana Alhamisi, tarehe 13 Februari 2020, liliitisha mkutano na waandishi wa habari jijiji Dar es Salaam, kushinikiza serikali kuwarejesha nchini, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waishio nchini China.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Pambalu amesema, hatua ya serikali kushindwa kuwarejesha raia hao nchini, ni kinyume na matakwa ya Katiba, inayoelekeza serikali kulinda raia zake, kufuatia ukibuka kwa kirusi hatari cha Corona.

Mwandishi mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii, Thadei Ole Mushi, anachambua kauli hiyo ya Bavicha na kuonya, kwamba  ni hatari kwa serikali kuchukua hatua hiyo. Je, unajua kwa nini mwandishi anaonya kutochukuliwa kwa hatua hiyo? Fuatilia…

BARAZA la Vijana la taifa (BAVICHA), limetaka serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuwaresha nchini, rais wake waliopo nchini China. Mwenyekiti wa baraza hilo taifa, John Pambalu, amedai kuwa hatua ya serikali kushindwa kuwarejesha nchini raia wake hao, nio kinyume na utu na Katiba ya Tanzania.

Binafsi, sidhani kama hawa vijana wamewaza sawasawa. Kama kipindupindu chenyewe tumeshindwa kukizuia: Je, hiki kirusi cha Corona kikifika hapa nchini, tunaweza kukizuia? Si tutakufa kama mende wa chooni?

Watu wa mwisho waliosafiri toka Wuhan China kuelekea Japan wameshailetea Japan balaa kubwa na wengine wamezuiwa kwenye meli.

Shirika la Afya ulimwenguni (WHO), inapambana ugonjwa huu usienee kila mahali duniani kwa kuwa ukianza kuenea kila mahali watashindwa kabisa kuucotrol na litakuwa janga la dunia nzima.

Watu wa Wuhan wenyewe hawaruhusiwi kusafiri kwenda maeneo mengine ya China kuzuia kusambaa; Bavicha wao wanataka tuwalete wenzetu.

Ni kweli ni ndugu zetu. Lakini kwa ukubwa wa jambo hili, Bavicha hawajafikiria vizuri. Si kila jambo ni la kukosoa uamuzi wa serikali; kisa tu, ninyi ni wapinzani.

Nilitegemea mje tofauti na UV-CCM kwa hoja zenye mashiko ila hizi maski mlizoanza kuvaa sijui mtaishia wapi. Ninyi na UV-CCM, ni Pipa na Mfuniko.

Huyu Pambalu asipopatiwa wasaidizi wenye uelewa, BAVICHA itakuwa inatoka uchi kila Siku. Hili kwenye mpira huwa tunaita “BOKO” na hapa bila kumung’unya maneno, “Pambalu katoa Boko.”

Huyu ana tofauti gani na yule aliyesema, “Zitto ashughulikiwe?”

Ole Mushi

0712702602

error: Content is protected !!