April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya ‘kimapinduzi’ yasogezwa mbele

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

KESI iliyofunguliwa na Ofisa wa Mtandao wa Haki za Binaadamu (THRDC), Paul Kisabo kupinga washtakiwa wa makosa ya uhujumu kunyimwa dhamana, imesogezwa mbele. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo namba 35 la mwaka 2019,  iliyopo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilianza kutajwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Februari 2020.

Shauri hilo lililopo mbele ya majaji watatu ambao ni Jaji Dk. Benhajj Masoud, Jaji Magoiga na Jaji Juliana Masabo, limeahirishwa mpaka tarehe 25 Februari 2020.

Kisabo ambaye ni Mwanasheria wa THRDC, aliwakilishwa na Wakili Daimu Halfani na Jeremiah Mtobesya ambapo waliieleza mahakama, kuwa bado hawajapata majibu ya maombi kutoka upande wa mjibu maombi.

Wakili wa Serikali Abubakar Mrisha akisaidiwa na Vivian Method, aliieleza mahakama kuwa, wamechelewa kujibu maombi hayo baada ya kuchelewa kupata baadhi ya taarifa kutoka kwa Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa serikali (DPP) ambazo zingewezesha kujibu maombi hayo, na kuwa taarifa hiyo waliipata baada ya siku  14 za kujibu maombi hayo.

Majaji katika kesi hiyo, wameutaka upande wa Jamhuri kujibu maombi hayo ndani ya siku saba kuanzia siku ya leo, shauri hilo lilipotajwa.

Mwanasheria Kisabo amefungua shauri hilo kupinga Kifungu namba 148(5)(d)(v) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, ambacho kinazuia watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kupewa dhamana, na kwamba ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma na Julai 2019, alitoa pendekezo kuwa kesi zote ziwe na dhamana na kwamba, kesi za uhujumu uchumi zinachukua muda mrefu bila upelelezi kukamilika licha ya sheria kutamka wazi muda gani unatakiwa ili kukamilisha upelelezi.

Msingi wa shauri la Kisabo ni kupinga kifungu namba 148 (5)(d) (v) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 (Toleo la mwaka 2002), ambacho kinazuia mtuhumiwa wa uhujumu uchumi kupewa dhamana kinyume na ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kifungu hicho kinakiuka moja kwa moja ibara ya 4 (1) na (2), Ibara ya 13 (4) & (6) (a)(b) na (d), Ibara ya 15 (1) na Ibara ya 17 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kifungu namba 148 (5) (d) (v) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinakiuka haki za msingi za mtuhumiwa ikiwemo;

Haki ya kupata dhamana, haki ya kuchukuliwa bila hatia mpaka pale mahakama itakapothibitisha, haki ya kuwa huru, haki ya kutokubaguliwa mbele ya sheria na haki ya kusikilizwa kesi yake kwa wakati

Aidha, Kisabo amedai kifungu hicho, kinakiuka haki zingine za mtuhumiwa kama vile; haki ya usawa mbele ya sheria, haki ya kuheshimiwa utu wake, haki ya uhuru wa kutembea, haki ya kupata dhamana na pia kinaminya mgawanyo wa madaraka kati ya mhimili wa Bunge na Mahakama.

error: Content is protected !!