RAIS Samia Suluhu Hassan ameendelea kupangua Idara ya Usalama wa Taifa baada ya leo Jumatatu kumteua Balozi Ali ldi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Balozi Siwa amechukua nafasi ya Said Hussein Massoro ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa miezi saba peke yake kuanzia tarehe 3 Januari mwaka huu.
Balozi Siwa ameapishwa leo tarehe 28 Agosti 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na kuchukua nafasi ya Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Siwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) nafasi ambayo aliteuliwa na Rais John Magufuli mwaka 2018 kisha mwaka 2021 Rais Samia akamuongezea muda.
Awali kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.
Leave a comment