Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko TRA yazindua kampeni ya kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti
Habari Mchanganyiko

TRA yazindua kampeni ya kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA, Mkoa wa Kikodi wa Kariakoo wamebandika stika maalumu kwaajili ya uzinduzi rasmi wa kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapouza bidhaa zao na wananchi kudai risiti ambayo itakuwa thamani sawa na bidhaa waliyonunua kwa maendeleo ya Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa maalumu kwaajili ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mashine za kieletroniki (EFD) kwa wafanyabiashara nchini.

“Unapouza toa risiti na vile vile unaponunua bidhaa udai risiti yako.”

Amesema kuwa wamebaini kuporomoka kwa utoaji wa risiti kwa sababu risiti zinazotolewa zimekuwa tofauti na matarajio nayo inapelekea makusanyo kushuka.

Beyanga amefafanua faida za kutoa na kudai risiti pale biashara inapofanyika kuwa inasaidia kutunza kumbukumbu, inasaidia katika ukadiliaji wa mapato yanayoendana na uhalisia wa biashara ambayo mfanyabiashara amefanya pamoja na kuchangia pato la taifa.

Amesema kampeni ya uhamasishaji wa wafanyabiashara kutoa risiti na wananchi kudai risiti ni endelevu hivyo jamii inatakiwa kutekeleza bila shuruti.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boss Shopping Centre, Hanif Janmohamed amesema kuwa amejisikia vizuri kwa TRA kuendelea kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa kutoa risiti halali kulingana na bidhaa iliyonunua.

“TRA sasa hivi wanafanya vizuri, hakuna Harasment kama zilizokuwa zamani, sasa hivi maisha yanakwenda vizuri, pia tunaelimishana kwenye sehemu ambazo zinachangamoto.” Amesema Janmohamed

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi pia amesema kuwa kutoa na kudai risiti ni wajibu wa kila mmoja kwa maendeleo ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!