Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaanza kuchochea moto uchaguzi serikali za mitaa
Habari za Siasa

Chadema yaanza kuchochea moto uchaguzi serikali za mitaa

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kutumia mikutano yake ya hadhara kuwataka wananchi kutumia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024, kung’oa mizizi iliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia wenyeviti wa vitongoji na serikali za mitaa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Leo tarehe 28 Agosti 2023, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, amerudia kuwaomba wananchi kutochagua wagombea wa CCM katika uchaguzi huo na Uchaguzi Mkuu wa 2025, ili kuweka viongozi watakaolinda maslahi yao.

“Kuna yeyote anayeamini kwamba tukiendelea na CCM maisha yake yatakuwa mazuri? Hapana, kwa hiyo kama tunataka nafuu kwenye nmaisha yetu tuondoe hii toa toa (kuhamisha wananchi katika baadhi ya maeneo) na hatuwezi kuindoa bila kuiondoa CCM,” amedai Lissu na kuongoza:

“Kwa hiyo kama tunataka nafuu tuanze na CCM, hawa vijiji watendaji wa kijiji, tukiwaondoa nani atakayeleta mgambo nyumbani kwako? Mwenyekiti wa Chadema atasema hakuna toa toa. Tumalizane na CCM, tusipoimalizana na CCM watatumaliza.”

Wito huo wa Lissu, alishawahi kuitoa katika mikutano yake ya hadhara, akiwataka wananchi kujiunga na Chadema, akidai kuwa chama hicho kitasaidia kuweka mifumo itakayoimarisha maisha yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!