Friday , 29 September 2023
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: CCM mmerogwa?

Mbowe akihutubia mkutano
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiikabidhi Chadema Serikali kama kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi kwa maslahi ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Mbowe ametoa wito huo leo tarehe 28 Agosti 2023, katika mkutano wa hadhara wa Chadema, uliofanyika Kishapu mkoani Shinyanga, wakati akizungumzia mkataba wa uwekezaji wa bandari, uliofungwa kati ya Serikali ya Tanzania na Imarati ya Dubai.

Mwanasiasa huyo amehoji iwapo kama CCM imerogwa, hadi kupelekea kutaka kukabidhi uendeshaji wa bandari nchini kwa kampuni ya kigeni ya Dubai Port Wolrd (DP Wolrd), wakati rasilimali hiyo ni lango la uchumi wa nchi kwa kuwa inategemewa na nchi jirani zisizokuwa na bandari.

“Wanataka kumpa mwarabu bandari zote kwa mkataba wa milele, tunauliza Serikali yetu mnampaje mgeni? Nchi jirani zinaitegemea bandari ya Tanzania, lakini tunachukua bandari zetu mnamkabidhi milele, tunawauliza CCM mmerogwa?,” alisema Mbowe.

Mbowe amesema “Kama mmerogwa mmerogwa huyo aliyewaroga labda kafa. Mnakwendaje kugawa rasilimali na urithi wa nchi yetu? Mnasema bandarini kuna wizi tumeshindwa kuendesha. Tunawaambia CCM kama wameshindwa kuendesha bandari zetu waikabidhi serikali kwa Chadema tuna uwezo wa kuendesha bandari zetu kwa kutumia watanzania wetu.”

Katika hatua nyingine, Mbowe amedai Serikali ya CCM imeshindwa kutumia kikamilifu rasilimali za nchi, ikiwemo madini na gesi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, huku akidai wananchi waishio katika mikoa yenye rasilimali hizo wanaongoza kwa kuwa masikini.

Katika nyakati tofauti, Serikali imetoa ufafanuzi juu ya dosari zinazoibuliwa na wapinzi dhidi ya mpango wake wa kuipa DP World kazi ya kuendesha baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam, ambapo imesema kampuni hiyo haitapewa mkataba wa milele, kama inavyodaiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!