Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Aweso akaribisha kampuni za India kuwekeza sekta ya maji
Habari Mchanganyiko

Aweso akaribisha kampuni za India kuwekeza sekta ya maji

Spread the love

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amezikaribisha kampuni za India kuja kuwekeza katika kuboresha zaidi miundombinu ambayo itasaidia kukuza uchumi wa Tanzania hususani katika Sekta ya Maji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Aweso ametoa wito huo wakati akichangia mada katika mdahalo uliokuwa na mada ya “Miundombinu Thabiti ya Dunia Katika Ukuaji wa Uchumi” uliofanyika wakati wa Mkutano wa 17 wa Ushirikiano baina India na Afrika.

Mkutano huo ambao umeratibiwa na Confederation of Indian Industry-Exim Bank Conclave unahusu namna bora ya kuendeleza ushirikiano na fursa za ukuaji wa kiuchumi kati ya India na Afrika.

Wakati wa Mdahalo huo Waziri ameeleza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kujenga miundombinu thabiti katika kuhakikisha inaimarisha uchumi wake.

“Baadhi ya miundombinu aliyoeleza ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, ujenzi wa miradi ya maji, ujenzi wa barabara pamoja na kuimarisha bandari na viwanja vya ndege,” amesema Aweso

Amesema, jitihada inayochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wa miradi hiyo utasaidia sana katika ukuaji wa uchumi kwa kuwa itarahisisha uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa.

Aidha, ameelezea mchango wa sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa kushirikiana na serikali kwani utarahisisha ukuaji wa uchumi.

Vilevile, ameiomba Serikali ya India kuendelea kuunga mkono jitihada za Tanzania katika ujenzi wa miundombinu katika sekta tofauti.

Mdahalo huo, pia uliwahusisha Emile Ouosso waziri wa Viwanda na uwekezaji kutoka Jamhuri ya Congo, Abid Said Mia Waziri wa Maji kutoka Malawi, Sridharan Madhusudhanan, kutoka India Siding Maiva Bank ya Maendeleo Afrika na Tejaswi Avasarala kutoka Nigeria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!