August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Haji Manara afungiwa miaka miwili, faini Sh20 Mil.

Spread the love

 

KAMATI ya maadili ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemfungia msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara, kujihusisha na mchezo wa soka katika kipindi cha miaka miwili ndani na nje ya nchi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mbali na kifungo hicho pia Manara atalazimika kulipa faini ya Sh20 milioni.

Uamuzi huo umetolewa hii leo tarehe 21 Julai 2022, Jijini Dar es Salaam na kusomwa na Katibu wa Kamati hiyo, Walter Lungu.

Katika maamuzi hayo kamati ilieleza kuwa Manara alikutwa na hatia katika makosa yote mawili aliyoshtakiwa nayo mbele kamati hiyo.

“Kamati imemtia hatiani mara baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mlalamikaji na utetezi wa mlalamikiwa.

“Ndugu Haji Manara anafungiwa kujihusisha na mchezo wa mpira wa miguu ndani na nje ya nchi katika kipindi cha miaka miwili pamoja na faini ya shilingi milioni 20.” Alisema katibu huyo wa kamati

Aidha katika uwamuzi huo, kamati hiyo ilieleza kuwa adhabu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia leo tarehe 21 Julai 2022, huku pande zote zikipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 21.

Msemaji huyo wa klabu ya Yanga alishtakiwa mbele ya kamati hiyo kwa makosa mawili, ikiwemo ukosefu wa maadili kwa Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam, uliopigwa Tarehe 2 Julai 2022, jijini Arusha.

Kosa la pili ni kumtishia Karia kwa kumtolea maneno ya dhihaka huku akijua fika ni kosa la kimaadili na kuichafua taswira ya TFF.

Manara aliingia kwenye mvutano huo wakati wa mapumziko kwenye mchezo huo wa fainali kati ya Yanga, dhidi ya Coastal Union, wakati ambao Yanga ilikuwa nyuma kwa bao 1-0.

error: Content is protected !!