Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Auawa kwa shoka, kisa wivu wa mapenzi
Habari Mchanganyiko

Auawa kwa shoka, kisa wivu wa mapenzi

Kamanda wa Polisi Morogoro, Wilboard Mutafungwa
Spread the love

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti akiwemo mwanamke mmoja Rose Mngwe (43) mkulima na mkazi Njage wilayani Kilombero kuuawa kwa kukatwa na shoka kichwani na mumewe kwa wivu wa mapenzi. Anaripoti¬† Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Wilboard Mutafungwa amesema hayo leo tarehe 1 Agosti, mwaka huu, ofisini kwake kuwa tukio la kwanza lilitokea 28 Julai, saa 3 asubuhi ambapo mwanamke huyo aliuawa na mumewe Jacob Kambo (45) mkazi wa kijiji cha Njage.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa mwanaume huyo baada ya kumuua mke wake Rose kwa shoka kichwani aliamua kukimbilia porini na kwenda kujinyonga kwenye mti kwa kutumia kamba.

Kamanda huyo amesema inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliamua kufanya tukio hilo baada ya kuona mkewe hakumsikiliza alipomwambia kuwaondoa watoto wake wakike aliowazaa nje ya ndoa yao ili waende kwa wazazi wenzao waliowazalisha watoto kwa madai kuwa wanawanyima nafasi wakiwa hapo.

Amesema, miili ya marehemu hao imeshakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi.

Katika tukio la pili, Leo Charles Mashaka (61) mkazi wa kitongoji cha Igagafu wilayani Kilosa ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni na mtoto wake wa kumzaa aitwaye Emmanuel Leo Charles chanzo kikidaiwa kuwa ni kudai urithi.

Kamanda Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea tarehe 30 Julai, saa 11 alfajiri katika kata ya Lumuma Tarafa ya Idete wilaya Kilosa ambapo baba huyo alimpigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni upande wa kulia na kusababisha jeraha na michubuko mgongoni na mtoto wake huyo chanzo kikiwa ni ugomvi wa kifamilia akigombea urithi.

Kamanda huyo amesema, mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi utakapokamilika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!