Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amwibua Mbwa wa Lugola
Habari za Siasa

Zitto amwibua Mbwa wa Lugola

Spread the love

SIKU moja baada ya Zitto Kabwe, kumweleza Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwamba, ashughulike na mbwa wa polisi, hatimaye majibu yamepatikana leo alipo mbwa huyo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Jana Julai 30, 2018 wakati akijibu agizo la kujisalimisha kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Lindi kwa tuhuma za uchochezi, Zitto alisema kuwa haendi na mwisho wa taarifa yake kwenye ukyrasa wake wa twetter aliandika “…Nashauri Waziri ampate kwanza yule Mbwa wa Polisi Bandari.”

Leo mbwa huyo wa kazi maalum za Bandari ya Dar es Salaam aliyedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, anatakwa kupelekwa alikuwa kwenye mafunzo katika Bwalo la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa katika mkutano na wanahabari.

Amezungumza hayo huku ukumbini hapo kukiwa na mbwa wawili wa polisi, akiwamo anayedaiwa kutoweka.

Amesema kulikuwa na mkanganyiko na hakuna mbwa aliyepotea.

“Tunataka kuwaambia kuwa, mbwa huyo alikuwa kwenye mafunzo ya Bwalo la Polisi na mbwa aliyekuwa hayupo siyo hobi,” amesema Mwakalukwa na kuongeza:

“Mbwa wote wapo hakuna hata mmoja aliyetoweka huwa wanaenda kwenye kazi na kurudi.”

Julai mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alimpa saa saba Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro kuhakikisha mbwa huyo anarudi bandarini baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!