Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kujiuzulu Meya Ilala, CUF pachimbika
Habari za SiasaTangulizi

Kujiuzulu Meya Ilala, CUF pachimbika

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) kumewaka baada ya aliyekuwa Naibu Meya wa Ilaya anayetokana na chama hicho, Omary Kumbilamoto leo Agosti mosi, 2018 kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kambi ya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na ile inayoongozwa na Prof. Ibrahim Lipumba zimeanza kutuhumiana kuhusika na mkakati wa Kumbilamoto kukimbilia CCM.

Wakati kambi ya Maalim Seif ikimtuhumu Prof. Lipumba kuhusika na mkakati wa kudhoofika UKAWA, upande wa Prof. Lipumba umejibu mapigo.

Kumbilamoto ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Vingunguti iliyopo katika Halmashauri ya Ilala, jijini Dar es Salaam amejivua uanchama wa CUF leo sambamba na wadhifa wa Naibu Meya katika Halmashauri ya Ilala leo.

Kumbilamoto ameeleza kuwa, sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kupewa vitisho kutoka kwa viongozi wa CUF kutokana na kitendo chake cha kushirikiana na serikali katika kutekeleza majukumu ya wananchi.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF ambaye ni Kambi ya Maalim Seif, Shaweji Mketo amemtuhumu Prof. Lipumba na watu wake kuhusika na vitisho vinavyodaiwa kutajwa na Kumbilamoto.

“Uongozi unaozungumziwa ni wa Prof. Lipumba sio wa sisi tunaoamini kama chama taasisi, kama madai ni hayo uongozi unaodaiwa kufukuza uanachama muda mwingi umekuwa ukifanya hivyo ni wa Lipumba,” amesema na kuongeza Mketo;

“Kama madai yake ni kweli maana yake ni kwamba anakubaliana na Lipumba sababu kazi yake ni kusaidia Chama cha Mapinduzi CCM. Hayo mazingira ya kufukuza wanachama, kuwaondoa wabunge wetu Lipumba ndio amefanya hivyo kwa kuondosha watu kwenye nafasi zao.

“Kama mtendaji wa chama ninachoamini Lipumba na genge lake ni kusaidia ccm, na kuhama maana yake ni kuunga mkono juhudi za Lipumba kukisaidia ccm.”

Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Prof. Lipumba amesema, kundi la Maalim Seif halisemi ukweli.

Amesema, Mketo na Kumbilamoto hawana ushahidi wa hayo wanayoyaeleza na kwamba, kama wana ushahidi wowote wa vitisho, wauweke hadharani.

“Kumbilamoto ni mamluki, hana lolote hajapewa vitisho vyovyote, amekubali kuwa bidhaa akaenda sokoni akafika bei akakubali kununuliwa.

“Mimi nilikuwa nawasiliana na Kumbilamoto, asitafute sababu ambayo haipo. Asilete visingizio vya ajabu ni udhaifu wake na suala la fedha, na kama leo nimeshangaa hiyo taarifa ya kujiunga na CCM,” amesema Sakaya.

Sakaya ameeleza kuwa “hayo madai ndiyo maana unasema huenda, anafanya kazi kwa hisia na mimi sifanyi kazi kwa hisia mwambie akupe ushahidi alipewa vitisho na nani na alete barua.

“Katiba yetu inataka kumpa mtu barua Kumbilamoto hajawahi kupata barua wala onyo wala ya kuitwa, na wale waliofukuzwa walipewa barua wakakataa ndio tukawavua uanachama,”amesema.

Yeye ambacho kama madai ni hayo uongozi wa juu wa kudai kufukuzwa uanachama, sio wa taasisi ni wa bwana lipumba, kama madai yake ni kweli maana yake ni kwamba anakubaliana na matakwa ya lipumba na lipumba anatekeleza matakwa ya ccm kama madai ya ni sahihi mimi binafsi anachofanya

Kama anaamua kujivua uanachama, maana yake ni kukubaliana na lipumba kudhoofisha

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!