Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Magufuli mgeni rasmi mkutano wa ALAT
Habari Mchanganyiko

Rais Magufuli mgeni rasmi mkutano wa ALAT

Mwenyekiti wa ALAT, Gulamhafeez Mukadamu
Spread the love

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) intarajia kufanya mkutano wake mkuu wa 34 Desemba 24 hadi 28 mwaka huu Jijini Dodoma huku mgeni rasimi akiwa Rais John Magufuli. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Katika mkutano huo wanatarajia kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuona ni namna gani ya kuishauri serikali juu ya urudishwaji wa vyanzo vya mapato vilivyochukuliwa na serikali kuu na kuzifanya halmashauri nyingi kuwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Hali ya halimashauri nyingi kuwa na uchumi kiduchu unatokana na serikali kuchukua vyanzo vingi vya mapato na kuviingiza katika serikali kuu jambo ambalo lilioneonekana kuwa kikwazo cha maendeleo katika halmashauri nyingi kwa kushindwa kuwa na vyanzo vya mapato vya kutosha kama ilivyokuwa hapo awali.

Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadamu alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mkutano huo ambao utafanyika katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete jijini hapa.

Amesema kuwa Jumuiya ya Tawala ya Mitaa Tanzania ni chombo wakilishi na sauti ya pamoja ya Mamlaka ya serikali za mitaa inayounganisha halmashauri zote za majiji, manispaa, miji na wilaya Tanzania Bara na kueleza kuwa jumuiya hiyo ilianzishwa Jijini Dodoma 13 Desemba 1984 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa serikali za mitaa kwa sheria sura Na.287 na 288 ya sheria ya Tanzania.

“Majukumu ya msingi ya Jumuiya kwa mujibu wa katiba yake ni kuwakilisha haki maslahi ya serikali za mitaa katika vyombo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, kushawishi mabadiliko ya sera na sheria kwa lengo la kuwezesha utekelezaji mzuri wa dhana ya kupeleka madaraka kwa wananchi.

“Kiusaidizi kwa mamlaka ya serikali za mitaa katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwa jukwaa la upashanaji wa habari na kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” alisema Mukadamu.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!