Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Mwamakula aitisha maombi kumuombea Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Mwamakula aitisha maombi kumuombea Mbowe

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Emmaus Mwamakula
Spread the love

 

MKUU wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Askofu Emmaus Mwamakula, ameitisha maombi maalumu ya siku saba, kwa ajili ya kumuombea Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aliyeko mahabusu kwa tuhuma za ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Mwamakula ameitisha maombi hayo jana tarehe 26 Julai 2021, akiwataka Watanzania, wamuweke Mbowe mbele za Mungu, kufuatia kipindi kigumu anachokabiliana nacho akiwa mahabusu, katika Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Askofu Mwamakula alielekeza maombi hayo yaanze jana Jumatatu hadi tarehe 2 Agosti 2021.

“Tunatangaza maombi ya siku saba mfululizo kwa ajili ya kumuombea Mbowe kuanzia Jumatatu. Watu wakusanyike katika vikundi majumbani au watumie muda wa maombi kila siku, kabla ya kulala wakilitaja jina la Mbowe mbele za Mungu. Neno la kusimamia ni Zaburi 20:7,” ameandika Askofu Mwamakula.

Mbowe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana tarehe 26 Julai 2021 na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na ugaidi.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Mbowe anadaiwa kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

Mwanasiasa huyo alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Martin, akisaidiwa na Tulimanywa Majigo.

Inadaiwa kuwa, Mbowe alitenda makosa hayo kati ya Mei na Agosti 2020, kwenye Hoteli ya Aishi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kesi ya Mbowe, inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 5 Agosti 2021, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha nyaraka muhimu katika Mahakama Kuu, kwa ajili kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo.

Mbowe alifikishwa mahakamani siku tano, tangu alipokamatwa akiwa katika Hoteli ya Kingdom jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai mwaka huu, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!