Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tanzania kupigwa jeki upimaji Korona, kujenga viwanda vya chanjo
AfyaTangulizi

Tanzania kupigwa jeki upimaji Korona, kujenga viwanda vya chanjo

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (CDC), Dk. John Nkengasong
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inatarajia kujenga viwanda vya kuzalisha chanjo za magonjwa ya mlipuko. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Jaffar Haniu.

Akitoa taarifa ya kikao cha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC), Dk. John Nkengasong, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kupitia taarifa hiyo, Haniu amesema, Rais Samia amemueleza Dk. Nkengasong kwamba Serikali yake itajenga viwanda hivyo, kupitia Mpango wa Tatu wa Taifa wa miaka mitano wa Maendeleo (FYDP III).

Mpango huo ulianza kutekelezwa Julai Mosi mwaka huu na unatarajiwa kufika tamati Juni 2026.

“Rais Samia amesema kupitia FYDP III, Serikali inakusudia kujenga viwanda vya kuzalisha chanjo za aina mbalimbali, katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,” imesema taarifa ya Haniu.

Taarifa ya Haniu imesema, kupitia kikao hicho kati ya Rais Samia na Dk. Dk. Nkengasong, walijadili namna ya kudhibiti Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19).

Imesema, Rais Samia amemhakikishia Dk. Nkengasong, kwamba Serikali yake itashirikiana na kituo hicho ili kukabiliana na ongezeko la kusambaa kwa ugonjwa wa UVIKO-19, kwenye nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

“Rais Samia amesema Africa CDC ni muhimu katika kusaidia kutoa elimu kwa wanadiplomasia wetu, ili kufahamu masuala ya afya na kuweza kushiriki kikamilifu, katika mikutano inayohusu masuala hayo katika maeneo yao,” imesema taarifa ya Haniu.

Aidha, Rais Samia amueleza Dk. Nkengasong, mikakati inayotekelezwa na Serikali yake katika kukabiliana na UVIKO-19, ikiwemo kuandaa kamati maalumu ya kitaifa ya kuratibu masuala yote yanayohusu ugonjwa huo.

“Rais Samia amesema mbali na kamati hiyo, Serikali imeboresha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya na utoaji wa elimu kwa umma, kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19,” imesema taarifa ya Haniu.

Kwa upande wake, Dk. Nkengasong, amesema Africa CDC iko tayari kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali, ili iweze kudhibiti ugonjwa huo.

“Dk. Nkengasong ametaja maeneo mengine ambayo Africa CDC inaweza kushirikiana na Tanzania kuwa ni kuzijengea uwezo maabara na wataalamu, ili kuimarisha upimaji na utambuzi wa aina mbalimbali za virusi vya UVIKO-19, pamoja na kusaidia masuala ya utafiti ,” imesema taarifa ya Haniu.

Aidha, Dk. Nkengasong amesema Africa CDC wameanzisha mpango wa Safari za Kuaminika utakaowawezesha wanachama wa AU kusafiri ndani na nje ya Bara la Afrika bila vikwazo vitokanavyo na ugonjwa wa UVIKO 19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Mabeyo awataje waliotaka kuzuia urais wa Samia

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the loveHUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia...

error: Content is protected !!