Marehemu Askofu Alfred Maluma wa jimbo katoriki Njombe
Spread the love
ASKOFU Alfred Maluma wa Jimbo Katoliki la Njombe nchini Tanzania, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Padri Justin Sapula wa Jimbo Katoliki la Njombe amesema, Askofu Maluma alifikwa na mauti saa 6:40 usiku wa 6 Aprili 2021 na taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Kufuatia kifo hicho, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa waumini wa Kanisa Katoliki na wananchi wa Njombe.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika “nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe Mhashamu Baba Askofu Alfred Maluma.”
“Alikuwa mtu mwema, mpenda maendeleo na aliyekuwa tayari kushirikiana na Serikali wakati wote. Nawapa pole Wakatoliki wote, Wananjombe na wote walioguswa na msiba huu,” amesema Rais Samia
More Stories
Mama mzazi wa IGP Sirro afariki dunia
CAG: Nyaraka za kughushi zilitumika Jeshi la Zimamoto
CAG: TGFA yatumia Bil. 3 kutengeneza ndege isiyotumika