May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kufungiwa Mwakalebela, Yanga yaikomalia TFF

Frederick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema kuwa haujaridhishwa kufungiwa kwa miaka mitano kwa Makamu Mwenyekiti wao, Fredrick Mwakalebela baada ya kukutwa na hatia na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwakalebela alifungiwa miaka mitano na kupigwa faini ya shilingi milioni saba, baada ya kukutwa na hatia katika makossa mawili ikiwemo kushindwa kuthibitisha madai ya kuwa vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini kuihujumu klabu ya Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imeeleza kuwa imepokea kwa mshtuko taarifa hiyo ya kufungiwa kwa kiongozi wao iliyotolewa Ijumaa tarehe 2, machi 2021.

Yanga wamesema kuwa kufungiwa kwa kiongozi huyo ni kama vitisho na kuufunga mdomo uongozi wa Yanga juu ya masuala yake muhimu yaliyowasilishwa TFF.

Aidha taarifa hiyo imendelea kueleza kuwa klabu hiyo inasubiri kupokea taarifa rasmi kutoka TFF ikiwemo hukumu ya shauli hilo ili kukata rufaa na kuchukua hatua nyingine.

Katika taarifa iliyotoka TFF kuhusu kufungiwa kwake ilieleza kuwa Mwakalebela alishindwa kuthibitisha shutuma za kuwa TFF, Bodi ya Ligi na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi kuwa inahujumu klabu ya Yanga.

error: Content is protected !!