Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Anne mkosoaji wa Kagame afariki, kifo chaibua utata
KimataifaTangulizi

Anne mkosoaji wa Kagame afariki, kifo chaibua utata

Anne Rwigara
Spread the love

Anne Rwigara (41), aliyekuwa mkosoaji wa Serikali ya Rwanda na mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa zamani nchini Rwanda, Assinapol Rwigara amefariki dunia nchini Marekani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Anne amefariki duniani saa chache baada ya kueleza kupatwa na maumivu makali ya tumbo.

Diane Rwigara

Anne ambaye alikuwa dada wa Diane Rwigara mwanamke pekee aliyetaka kugombea urais nchini Rwanda mwaka 2017, alifahamika zaidi baada ya kukamatwa yeye, dada yake Diane na mama yao.

Wanafamilia hao watatu walikaa gerezani kwa siku kadhaa mwaka 2017 baada ya uchaguzi wa urais wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukwepaji kodi na kupelekea mali za familia, kikiwemo kiwanda cha tumbaku na akaunti za benki kushikiliwa.

Anne Rwigara enzi za uhai wake.

Anne alishtakiwa kwa kosa la kukusudia kusababisha machafuko, kufanya uhalifu alioshirikiana na kaka yake na mama yake na mashtaka mengine.

Hata hivyo, baadaye Anne aliachiliwa na mahakama, lakini dada yake mkubwa Diane, ambaye alitaka kuwania urais, na mama yake Adeline walikaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Reuters, mama yake Anne amesema chanzo cha kifo cha mwanaye ni fumbo kwani bado wanatilia mashaka mazingira ya tukio hilo.

Kifo cha baba yake mwaka 2015, pia kilijawa na utata ambapo familia yake ilidai aliuawa katika ajali iliyopangwa na kumwandikia barua Rais Paul Kagame wakitaka uchunguzi ufanyike juu kifo cha Assinapol.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!