October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Amuuwa nduguye kisa Sh. 1,500

Pingu

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, kwa tuhuma za kumuua ndugu yake, William Shoo (43), kwa kumjeruhi na kitu chenye ncha kali kichwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumatano, tarehe 13 Oktoba 2021, mkoani Kilimanjaro, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Simon Maigwa, amesema tukio hilo limetokea tarehe 10 Oktoba, mwaka huu, baada ya ndugu hao kugombana.

Kamanda Maigwa amesema, ugomvi wa ndugu hao uliibuka baada ya marehemu Shoo, kugoma kuchangia malipo ya nyama waliyokula pamoja, yaliyogharimu Sh. 1,500.

“Jeshi la Polisi Kilimanjaro linamshikilia mtuhumiwa mmoja jina tunalo, kwa tuhuma za mauaji ya ndugu yake aitwaye William Shoo, kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani, kwa kutaa kuchangia kulipia nyama ya 1,500 waliokula wote wawili,” amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema, mwili wa marehemu Shoo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mawenzi mkoani humo, kwa ajili ya uchunguzi wa daktari.

Na kwamba, mtuhumiuwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

error: Content is protected !!