RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Joe Biden wakati akimaliza ziara yake ya siku mbili nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Rais Kenyatta atakuwa rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana na kiongozi huyo wa Marekani, tangu Biden aapishwe kuwa rais wa taifa hilo, Januari 2021.
Msemaji wa Ikulu ya Kenya amesema, viongozi hao wawili watajadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya amani, usalama na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Jumanne, Rais Kenyatta aliwaongoza viongozi wa biashara kusaini mikataba kadhaa ya uwekezaji wa biashara ndogo na wastani pamoja na miradi ya usafirishaji na nishati safi.
Marekani inaiona Kenya kuwa mshirika sahihi katika kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki mwa Afrika.
Leave a comment