Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mabilioni ya IMF yatua Dodoma, RC Mtaka aonya wafanyabiashara
Habari za Siasa

Mabilioni ya IMF yatua Dodoma, RC Mtaka aonya wafanyabiashara

Anthony Mtaka, Mkuu wa mkoa wa Dodoma
Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka amewataka wafanyabiashara mkoani humo, kutopandisha bei za bidhaa za ujenzi na kuendelea na bei elekezi ya Serikali. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kupokea fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF), Sh.1.3 trilioni kwajii ya kupambana na ugonjwa wa corona.

Fedha hizo zimegawanywa kwenye mikoa mbalimbali ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa sekta ya afya, elimu na miundombinu ambapo Mkoa wa Dodoma umepata Sh.17.97 bilioni.

Leo Jumatano, tarehe 13 Oktoba 2021, RC Mtaka amekutana na wafanyabiashara na kuwaeleza fedha hizo ni fursa kubwa kiuchumi kupitia biashara kwani zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wakati na wadogo ili kuwainua.

Amesema fedha hizo zimetolewa lengo ni kwenda kuwanufaisha sekta binafsi na wafanyabiashara wadogo na wakati hivyo ni marufuku bidhaa za ujezi kupandishwa bei kiholela.

“Naendapo ikatokea au kujulikana nyinyi wafanyabishara mmepandisha bei kiholela, serikali ya mkoa itakwenda kununua bidhaa na vifaa vya ujenzi mikoa mingine,” amesema Mtaka

Pia, amesema kupitia fedha hizo sekta binafsi inakwenda kukua na hata uchumi wa mtu mmoja mmoja kwani kupitia fedha hizo kila kata imepitiwa na ujenzi wa miradi ya kimaendeleo.

“Sasa niwaombe wafanyabiashara, fedha zimetufikia sasa, tusilale tuchangamke soko hilo, masuala ya kulala unafungua duka saa sita mchana msije kumtafuta mchawi,” amesema RC Mtaka.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema fedha hizo ni fursa kubwa kwenye uchumi kupitia biashara kwani fedha hizo zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wakati na wadogo.

“Nataka mtambue fursa zinazokuja lengo tunataka kuzalisha wafanyabishara mamilionea na mabilionea kupitia fedha hizi, tunataka wafanyabishara wadogo wakue kikubwa tubadilishe bishara zetu,” amesema Profesa Kitila

Sambaba na hilo, Profesa Kitila amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia mambo makuu matatu amabayo kutosheleza mahitaji kama ni kukopa mikopo waende kukopa fedha kwenye taasisi za kifedha kwani soko lipo la kutosha na waache imani za kishirikina.

Pili, ni kuzingatia ubora kwani kumekuwepo na shida panapokuwa na mahitaji makubwa wafanyabishara wamekuwa wakichukua bidhaa bila kuzingatia ubora sasa kipindi hiki tutafuatilia ubora.

Tatu, ni kuzingatia maadili ambapo amewataka wafanyabiashara hao kusimama imara kwa kuuza bidhaa na kutoa listi tena ya mashine ya EFDs.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Dk. Fatuma Maganga amewataka wafanyabiashara hao kuweka bidhaa zenye ubora na wazinagatie mahitaji na matakwa ya jiji linavyotaka kwani kila halmashauri inalangi zake kwenye uezekaji wa mabati.

Kwa upande wake, Abdullah Taratibu, Mratibu wa vijana wafanyabishara mkoa wa Dodoma TCCAI, ameuomba uongozi wa mkoa kutoa ruhusa siku za Jumamosi wafanyabiashara wote wafungue matuka yao mapema.

“Ni kweli fursa ya fedha katika mkoa watu zimetufikia lakini na sisi wafanyabishara biashara tunabanwa kufanya biashara siku ya Jumamosi, kutakiwa lifungua maduka saa 4 wakati siku ya Jumamosi ndio siku kubwa ya biashara,” amesema kiongozi huyo.

1 Comment

  • Mwandishi, sijakuelewa.
    Utawala wa Mama Samia umepokea fedha za UVIKO-19 kwa nchi nzima au Dodoma peke yake?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!