Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa
HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love

 

MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba wake ameamrishwa na mahakama kulipia hasara za kifedha kwa uchungu wa kisaikolojia. Yameripoti Mashirika ya Kimataifa.

BBC imeandika kuwa Mahakama ya Kanungu ilisema kuwa Richard Tumwine alilipa Sh 9.4 milioni kwa ajili ya masomo ya sheria ya Fortunate Kyarikunda, pesa ambazo sasa atatakiwa kuzilipa pamoja na gharama za kesi.

Kwa kusitisha uchumba wao baada ya miaka minne, Hakimu Asanasio Mukobi aliamua kuwa Kyarikunda alikiuka ahadi na kusababisha madhara kwa Tumwine.

Mahakama ilisema kuwa ni “isiyo na maana, upotoshaji na ulaghai” kwa mshitakiwa kudai kuwa wazazi wake walimwambia asiolewe na mwanaume mzee sana, ikisema” alikuwa na wakati wote wa kukataa maombi ya mapenzi mapema na kuepuka kutumia pesa zake “.

Haijulikani iwapo Kyarikunda atakata rufaa dhidi ya hukumu.

Wakosoaji wanasema gazeti la Monitor kwamba hukumu ina kasoro kwasababu uchumba ni tofauti na ndoa ambayo inakubalika kisheria.

Wakati huo huo Sheila Kawamara, kutoka kikundi cha utetezi wa wanawake ED EASSI, anaonya kuwa wakati mwingine huwa kuna hali za unyonyaji ambapo mwanaume humpatia pesa mwanamke kwa sharti kuwa atamuoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!