Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri
Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love
MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert kairuki (HKMU), Ahlam Azam Mohamed, ametoa siri ya namna alivyofanikiwa kuhitimu akiwa na miaka 21. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Akizungumza na Nipashe jana mara baada ya mahafali ya 21 ya chuo hicho, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ahlam alisema alimaliza darasa la saba akiwa na umri wa miaka 13 na baada ya hapo hakuendelea na masomo ya darasani.

Alisema baba yake alikuwa akimletea walimu wa masomo mbalimbali nyumbani ambao walimfundisha kwa miezi hiyo minne na kumudu kufanya mtihani wa kidato cha nne katika shule ya Almuntazir kama mtahiniwa binafsi.

“Nilisomea nyumbani masomo ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha nne kwa miezi minne kisha kikasoma masomo ya kidato cha tano na sita ndani ya mwaka mmoja kwa hiyo nilimaliza masomo ya kidato cha sita nikiwa na miaka 15,” alisema

“Nilijaribu kujiunga na vyuo lakini majibu yalichelewa kwa hiyo nikalazimika kusubiri mwaka mzima nikaja kujiunga na masomo ya udaktari hapa Kairuki mwaka 2018 nikiwa na miaka 16 na nafurahi leo hii nimehitimu udaktari,” alisema

Alisema alivutiwa kusomea nyumbani baada ya kumuona  kaka yake amefanikiwa kusoma masomo hayo ya kidato kwanza hadi cha nne akiwa nyumbani na kufaulu kwenye mitihani yake.

Awali, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, alisema chuo kinaona fahari kwa mara ya kwanza kuwa na mhitimu mdogo wa fani ya udaktari kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Alisema mhitimu huyo Alham Azam Mohamed alijiunga na chuo hicho mwaka 2018 ambapo amekuwa akifanya vizuri zaidi kwenye masomo yake yote na kufanikiwa kupata Shahada ya udaktari.

“Tulijaribu kupekua pekua kwenye maeneo mbalimbali nchini kuangalia kama kwenye vyuo vya wenzetu hapa nchini kuliwahi kuwa na mhitimu wa fani ya udaktari mwenye umri kama huu lakini ilionekana kwamba mbali na HKMU,  hapa nchini huyu ni wa kwanza,” alisema

Kwenye mahafali hayo, wahitimu walikuwa 308 ambapo mhitimu mmoja alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Sayansi yaani Doctor of Science (Honoris Cause), 13 Stashahada ya Ustawi wa Jamii, 82 Stashahada ya Uuguzi, 14 Shahada ya Ustawi wa Jamii, 35 Shahada ya Uuguzi, 150 Shahada ya Udaktari wa Binadamu.

Wahitimu wawili walitunukiwa Shahada ya Uzamili ya udaktari wa binadamu katika tiba ya afya ya watoto, watatu Shahada ya Uzamili ya Upasuaji, watatu Shahada ya Uzamili ya Magonjwa ya wanawake na uzazi na sita Shahada ya Uzamili ya Tiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Spread the loveSERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu...

Elimu

St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne

Spread the love  WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari...

error: Content is protected !!