August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Algeria yajiita maskini jeuri

Mji Mkuu wa Algeria, Algiers

Spread the love

ALGERIA imesema haitachukua mkopo wa kigeni licha ya nchi hiyo kukabiliwa na matatizo mengi ya ndani hususani ya kiuchumi, anaandika Victoria Chance.

Uchumi wa nchi hiyo umeporomoka kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

Abdul Majeed Taboun Waziri Mkuu wa Algeria ameyasema hayo katika kikao na mkuu wa Jumuiya ya

Waajiri na Wafanyakazi wa nchi hiyo na kuongeza kuwa, Rais Abdelaziz Bouteflika wa nchi hiyo amepiga marufuku nchi yake kuchukua mkopo kutoka nje hadi pale taifa litakapokuwa halikabiliwi na hatari yoyote ile.

Aidha, amesema kuwa nchi hiyo inataka kuwa moja ya nchi zinazostawi kiuchumi kwa kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali.

error: Content is protected !!