Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo kuja kivingine 2022 kuibana Serikali nje ya Bunge
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo kuja kivingine 2022 kuibana Serikali nje ya Bunge

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)
Spread the love

 

BAADA ya Bunge la  12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukosa idadi kubwa ya wabunge wa upinzani, Chama cha ACT-Wazalendo, kinatarajia kuzindua mbinu za kuisimamia Serikali hususan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, nje ya mhimili huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe  25 Desemba 2021 na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa ya Zitto imesema kuwa, mbinu hizo zitazinduliwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho, utakaofanyika tarehe 29 Januari 2022.

Zitto ameandika, ACT-Wazalendo imeamua kuifuatilia miradi ya maendeleo ya Serikali, ili kuhakikisha fedha za umma pamoja na za mkopo kutoka Benki ya Dunia (W.B) na Shirika la Fedha Duniani (IMF),  zinazotumika zinaakisi thamani ya miradi husika.

“Kati ya Mwezi Machi na Desemba 2021, Benki ya Dunia imeidhinisha fedha kwa Tanzania jumla ya Dola za Marekani 2.3 bilioni, katika sekta mbalimbali. Sekta ya elimu ikiongoza kwa dola 1.43 bilioni,” ameandika Zitto.

Mwanasiasa huyo ameandika “bila ya Bunge madhubuti usimamizi wa fedha hizi na hata zile za IMF utakuwa mbovu. Sisi @ACTwazalendo tumeamua kufuatilia kila mradi na kuibua aina yeyote ya ubadhirifu.”

“Tunazindua mbinu mpya za kuisimamia Serikali nje ya Bunge kwenye Mkutano Mkuu Maalumu mwisho wa Januari 2022,” amesema Zitto.

Bunge hilo la 12 limebeba wabunge wengi wa Chama Tawala Cha Mapinduzi (CCM), ambao wako zaidi ya 320 huku vyama vya upinzani vikiambulia wabunge 25, wa majimbo watano (ACT-Wazalendo 4, Chadema 1) na viti maalum wasio na chama bungeni 19.

Idadi hiyo ya wabunge inatokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambayo yalikipa ushindi wa zaidi ya asilimia 90 CCM.

Pia, taarifa ya Zitto imesema ACT-Wazalendo kitazindua mkakati mpya wa siasa ili kuimarisha demokraisa uwajibaki na kuchochea mabadiliko.

Mbali na uzinduzi wa mikakati hiyo, taarifa ya Zitto imesema mkutano huo mkuu maalum wa ACT-Wazalendo, utatumika kumchagua Mwenyekiti wa chama hicho, ili kuziba pengo lililoachwa na Maalim Seif Shariff Hamad, aliyefariki dunia tarehe 17 Februari 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!