Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo kuichambua miswada ya uchaguzi
Habari za Siasa

ACT Wazalendo kuichambua miswada ya uchaguzi

Spread the love

Chama cha ACT Wazalendo kimeielekeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho kuichambua Miswada ya Sheria kuhusu Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 10 Novemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo. Ado Shaibu kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilala uliofanyika leo tarehe 12 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Simple Motel, Ilala, Dar es salaam.

“Ni jambo la faraja kuwa hatimaye miswada hii imewasilishwa Bungeni. Yapo masuala yaliyotufurahisha kama vile kuondosha suala la kupita bila kupingwa. Lakini, yapo masuala yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru, za haki na kuaminika.

Ado Shaibu


“Chama chetu kitafanya uchambuzi wa kina wa miswada yote mitatu. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama imeagizwa kufanya uchambuzi huo ambao utawasilishwa kwenye vikao vya Chama kabla ya kuwasilishwa Bungeni” alisema Shaibu.

“Tunapenda pia kurudia rai yetu kuwa itakuwa ni jambo la ajabu kwamba Tume ya Uchaguzi itayoundwa isisimamie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. ACT Wazalendo hatuungi mkono uchaguzi wa Serikali za Mitaa kusimamiwa na TAMISEMI” alisisitiza Ado.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo inaongozwa na Wakili Omar Said Shaaban ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar akisaidiwa na jopo la Mawakili wa Chama.

Mbali na hayo, Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na chaguzi katika ngazi ya majimbo akiweka bayana kuwa Ilala inakuwa Jimbo la 80 kukamilisha Uchaguzi.

“Mwezi Machi 2024, ni mwaka wa kukamilisha uchaguzi wa Chama ngazi ya Taifa. Hadi kufikia mwisho wa mwezi Desemba 2023, majimbo yote 264 yatakuwa yamekamilisha chaguzi zake. Baada ya hapo tutafanya chaguzi za Mikoa na mwishowe chaguzi za Taifa Mwezi Machi mwishoni” alihitimisha  Ado.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!