Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Biteko aagiza watumishi kufanya kazi zenye matokeo chanya
Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza watumishi kufanya kazi zenye matokeo chanya

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewasisitiza Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya kazi kwa ushirikiano ili kazi hizo zilete matokeo chanya kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Aliagiza hayo hivi karibuni wakati Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko walipozungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo katika kikao kilicholenga   kufahamiana, kujumuika pamoja, kujikumbusha majukumu ya kazi na kufanya Tathmini ya Utendaji Kazi ili kuongeza ufanisi.

Majaliwa aliwataka watumishi hao kuwahudumia Watanzania kwa weledi ili kuisaidia Serikali, kuwa wabunifu katika utendaji kazi, kusimamia Sera ya Uhifadhi wa Mazingira na kuwajibika kuwahudumia Watanzania.

Aidha, Dk. Biteko aliahidi  kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Ofisi hiyo katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali na kuwataka Watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano.

“Ninawaomba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mnifundishe, mnielekeze, na kuniombea ili tufanye kazi kwa pamoja kuwahudumia Watanzania na kazi hizo ziwe chachu ya kuboresha maisha ya Watanzania na kupunguza umaskini ,” alisema Dk.Biteko.

Kikao hicho kilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!