Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara TGC yaja na mpango wa kutengenexa mabilionea
Biashara

TGC yaja na mpango wa kutengenexa mabilionea

Spread the love

Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC) kimedhamiria kuhuisha mitaala ya mafunzo yake ili kutengeneza Watanzania matajiri  kupitia tasnia ya Uongezaji Thamani Madini.  Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumapili  jijini Dodoma na Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba, wakati akizungumza katika kipindi cha runinga na radio cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi Media.

Amesema kuwa katika kuhakikisha TGC inaendana na Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri, kituo hicho kimekuja na mkakati wa kuhuisha mitaala yake ili kutengeneza vijana na wanawake wengi kupitia mafunzo ya usonara kwa lengo la kuongeza thamani madini na kunufaika sio kwa kuchimba tu madini hapa nchini bali kuchonga, kuremba na kung’arisha mapambo kutoka kwenye miamba tofauti ya madini.

Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba

Ameongeza kuwa, TGC ina mkakati wa kuanzisha maabara ya Madini ya Vito itakayopatikana katika jengo jipya la taasisi hiyo litakalojengwa jijini Arusha sambamba na viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani madini ya vito yanayopatikana nchini kwa kwamba kwa kufanya hivyo itaongeza mchango wa madini hayo katika pato la taifa tofauti na yakisafirishwa nje ya nchi na kwenda kuongezewa thamani katika nchi nyingine.

Amewahimiza watanzania kujijengea hulka ya kununua urembo na mapambo yanayotokana na madini hayo yanayoongezewa thamani hapa nchini ili kusaidia vijana na wanawake wa kitanzania wanaofanya shughuli hizo kupata soko la uhakika lakini pia kutangaza bidhaa za kitanzania ndani na nje ya mipaka.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiunga na kituo hicho ili kujifunza mbinu za uongezaji thamani madini na kupata uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia taaluma hiyo hivyo kujipatia vipato sambamba kujiinua kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwa ujumla kupitia mnyororo wa uongezaji thamani madini.

Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC) kinapatikana jijini Arusha na kilianzishwa mwaka 2003, kwa lengo la kutoa mafunzo ya ndani kuhusu uchongaji miamba na madini ya vito kwa nia ya kuongeza ujuzi wa kuongeza thamani. Hivi sasa kituo hicho kinatoa mafunzo kwa ngazi ya Stashahada na Astashada kikiwa na malengo ya kuzalisha wahitimu wabunifu, wenye uwezo na wepesi ambao watakuwa na athari katika shughuli za uongezaji thamani madini hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!