Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: 2024 tutapigania maisha ya heshima kwa watanzania
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: 2024 tutapigania maisha ya heshima kwa watanzania

Spread the love

BARAZA la Mawaziri Kivuli la Chama cha ACT-Wazalendo, limeahidi kupigania maisha ya heshima kwa watanzania wanyonge, huku likianisha vipaumbele itakavyofanya 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 10 Januari 2024 na Waziri Mkuu Kivuli wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba mwaka uliopita ulikuwa wa mgumu sana kwa wananchi wa kawaida. Hali hiyo haijabadilika sana licha ya kuonyesha kwamba kuna hatua tumezifanya kama baraza ili kuleta nafuu kwa watu. Kwa mwaka huu tutaongeza jitiahada zaidi na kwa robo ya kwanza tutapigania zaidi mambo yanayogusa maisha ya watanzania,” amsema Semu.

Semu ametaja vipaumbele vyao kuwa ni, kuendelea kupigania unafuu wa gharama za maisha kwa kutoa mapendekezo  ya kudhibiti kupanda kwa bei za bidhaa. Kuishinikiza Serikali kutazama upya bei za nauli za mabasi na daladala nchini.

Vingine ni, kutopatikana kwa uhakika kwa huduma ya umeme (mgawo), kupigania haki na usalama wa ardhi kwa wananchi mijini na vijijini ili kumaliza migogoro ya ardhi nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!