Friday , 10 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Madadapoa kutoka TZ wafurika Rift Valley kuwakamua wakulima
Habari MchanganyikoTangulizi

Madadapoa kutoka TZ wafurika Rift Valley kuwakamua wakulima

Spread the love

KAMA ulidhani madadapoa hufurika mikoa ya Kanda ya Ziwa pekee pindi wakulima wanapovuna na kuuza pamba, umekosea kwani hali kama hiyo pia imetokea katika eneo la Rift Valley nchini Kenya ambapo inadaiwa kuwa kaunti za Bomet, Kericho, Kisii, Nandi na Mlima Elgon zimefurika akina dada hao wakati wakulima wa chai wakianza kupokea bonsai ya malipo yao wiki hii.

Vidosho hao wanaotajwa kutoka nchini Tanzania, Uganda na Kenya kwenyewe wamedaiwa kuendelea kumiminika mjini Kericho tayari kutafuna jasho la wakulima hao. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Migahawa ambayo kwa muda haikuwa ikipokea wateja wengi, kwa sasa imefurika huku nauli za magari ya abiria katika barabara za kuelekea Kisii na Kericho zikiwa zimepandisha.

Kwa wakazi maeneo hayo wamesema hiyo ni hali ya kawaida ambapo wanakiri kuwa warembo kutoka nchi jirani za Tanzania na Uganda, vilevile, wamekuwa wakijumuika na wenzao wa Kenya kuvuna.

Kwa upande mwingine, wakazi wa eneo la Konoin, Kaunti ya Bomet wameeleza kukerwa  na hali hiyo kwa madai kuwa makahaba wanatumia mitego mingi kuwanasa na kuwaibia wanaume.

“Badala ya kukodisha vyumba vya malazi mbali na mji, wanapangisha karibu na ploti zetu ili kuwadhibiti wanaume kwa muda mrefu, kuhakikisha wanawakamua kila kitu,” anasema Ann Chebet muuzaji wa mananasi eneo la Ngoina Road.

Aidha, kituo cha kibiashara cha Mogosiek kimedai vyumba vya kulala vimejaa na kuwalazimu baadhi ya walevi kutumia vichaka.

“Makahaba wachanga na wale wenye umri mkubwa hufika hapa mapema na kukodisha vyumba ambapo huwapeleka wateja wao,” anasema Robert Kipkemoi mkazi wa Mogogosiek.

Isitoshe wamiliki wa baa na migahawa wameongeza mtaji kutokana na mazingira mazuri ya kufanyabishara na wanatarajia idadi kubwa ya wateja.

Kipkemboi anasema ni jambo ambalo limekuwa likirudisha familia nyingi nyuma kimaisha.

Ikumbukwe kuwa Konoin ni eneo linalopatikana katika Kaunti ya Bomet ambapo idadi kubwa ya wakulima wa majani chai huwa wanatoka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

error: Content is protected !!