Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ashiriki misa kumuomba Mwalimu Nyerere
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ashiriki misa kumuomba Mwalimu Nyerere

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki misa ya kumuombea Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyefariki dunia tarehe 14 Oktoba 1999. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Misa hiyo imefanyika leo tarehe 14 Oktoba 2023, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Babati mkoani Manyara na kuongozwa na Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Antony Gasper Lwagen.

Mbali na Rais Samia, viongozi wengine walioshiriki misa hiyo ambayo inaenda sambamba na kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, ni Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango. Naibu Waziri Mkuu, Dotto Biteko. Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

Akizungumza wakati anaongoza misa hiyo, Askofu Lwagen aliwataka watanzania kumuombea Mwalimu Nyerere ili Mungu ampe pumziko la milele.

“Adhimisho hili ni la muhimu sana la kitaifa linalohusu kumbukizi ya siku ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwa namna ya kipekee naomba tumuombee na tutoe shukrani kwa Mungu kwa zawadi ya maisha yake ambayo imetufadhili kwa mengi,” amesema Askofu Lwagen na kuongeza:.

“Tunatumia nafasi hii kuiombea nchi yetu na raia wote tubaki kuwa na umoja, amani na mshikamano siku zote. Tunawaombea viongozi wetu wote wa dini na serikali kwa namna ya kipekee rais wetu Mungu aendelee kumpa afya na nguvu amjalie busara anayohitaji.”

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia, Dk. Mpango amesema watanzania wanamshukuru Mungu kwa zawadi wa Mwalimu Nyerere ambaye ni mwasisi wa uhuru, amani na mshikamano wa taifa.

“Tukumbuke wajibu wetu kwa taiofa letu, ndiyo namna bora ya kumuenzi na kubwa zaidi kulinda uhuru wa taifa lakini kukataa aina yoyote ya unyonyaji na ukandamizaji,” amesema Dk. Mpango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Potofu huzaa potoshi/ potoshi huzaa potofu?

Spread the loveDayosisi 7 za KKKT katika kanda ya Ziwa na Magharibi,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

error: Content is protected !!